Lengo
Kusimamia na kushauri masuala yote yanayohusu miundombinu katika Halmashauri.
Majukumu Kitengo kitafanya kazi zifuatazo:-
• Kushauri kuhusu masuala ya sekta ya ujenzi;
• Kupanga maendeleo ya miundombinu;
• Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo ya wakandarasi;
• Kukagua kazi za ujenzi zinazofanywa na Halmashauri na kuhakikisha ubora wake;
• Kutoa vyeti kwa wakandarasi kwa mikataba iliyokamilika;
• Kufanya uwekaji lami wa barabara mpya kwa kushirikiana na TARURA;
• Kuanzisha na kudumisha ushirikiano na Taasisi za nje na ndani ya Nchi zinazoshughulikia masuala ya miundombinu;
• Kushiriki katika kuwezesha utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi;
• Kusimamia mchakato wa ukuaji wa miji kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi; na
• Kusimamia maendeleo ya makazi vijijini na mijini kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya Ardhi.
Divisheni hii ina Sehemu tatu (3) kama ifuatavyo:-
• Sehemu ya Kazi;
• Sehemu ya Barabara; na
• Sehemu ya Maendeleo Vijijini na Mijini.
Sehemu ya Kazi
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:-
• Kutoa ushauri wa sheria, kanuni, taratibu na mambo yote yanayohusu ujenzi;
• Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni za masuala ya ujenzi;
• Kuandaa mikataba inayohusiana na majengo na mitambo;
• Kutayarisha na kukadiria gharama za ujenzi;
• Kufuatilia utendaji kazi wa wakandarasi;
• Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo kutoka kwa wakandarasi;
• Kukagua majengo na kuhakikisha ubora wake;
• Kutoa hati kwa wakandarasi kwa kazi zilizokamilika kulingana na mikataba; na
• Kusimamia uendeshaji wa warsha za Halmashauri.
Sehemu ya Barabara
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:-
• Kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohusiana na utambuzi na uwekaji lami wa barabara mpya;
• Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni kwenye barabara za lami;
• Kutengeneza barabara mpya katika ardhi iliyopimwa;
• Kuandaa mikataba ya uwekaji lami wa barabara mpya;
• Kutayarisha makadirio ya gharama za kuweka lami barabara;
• Kufuatilia utendaji wa wakandarasi;
• Kutoa hati kwa wakandarasi kwa kazi zilizokamilika kulingana na mikataba;
• Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo kutoka kwa wakandarasi;
• Kukagua barabara za lami ili kuhakikisha ubora; na
• Kusimamia ujenzi na matengenezo ya vituo vya mabasi.
Sehemu ya Maendeleo Vijijini na Mijini
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:-
• Kusimamia maendeleo ya makazi vijijini na mijini kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi;
• Kusimamia huduma za kimazingira na kijamii;
• Kuongoza mipango ya maendeleo ya miji, makazi na matumizi endelevu ya ardhi;
• Kusimamia na kuratibu usimamizi wa mambo ya kale na utalii;
• Kusimamia mchakato wa ukuaji wa miji kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi;
• Kuratibu na kukuza maendeleo ya miji inayochipukia kutoka vijiji hadi makazi ya mijini; na
• Kushiriki katika kuwezesha utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.