Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ni miongoni mwa Halmashauri 6 zinazounda Mkoa wa Simiyu zikiwemo Halmashauri ya Itilima, Busega , Meatu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Bariadi vijijini.Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ilianzishwa mwaka 1926 toka Mkoa wa Shinyanga na kujitegemea kama Halmashauri.
Wilaya ya Maswa ni kati ya Wilaya 5 zinazounda Mkoa mpya wa Simiyu. Wilaya nyingine zinazounda Mkoa wa Simiyu ni Bariadi, Busega, Meatu na Itilima. Kwa upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Meatu, Upande wa Kaskazini hadi Kaskazini Magharibi inapakana na Wilaya ya Itilima,Kusini hadi Kusini Magharibi inapakana na Wilaya ya Kishapu (Mkoa wa Shinyanga) na Upande wa Magharibi inapakana na Kwimba (Mkoa wa Mwanza).
Eneo la Wilaya ni kilometa za mraba 3,398 kati ya hizi 2,475 zinafaa kwa shughuli za kilimo na ufugaji, wakati kilometa za mraba 77 ni hifadhi ya misitu na kilometa za mraba 846 ni miinuko ya mawe, vilima na vichaka
Kiutawala, Wilaya ina tarafa 3, Kata 36 Mamlaka ya Mji 1 yenye vitongoji 40, pia kuna vijiji 120, na vitongoji 510.Halmashauri ina jumla ya Divisheni 9 na Vitengo 9.
i). Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
ii). Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
iii). Viwanda, Biashara na Uwekezaji
iv). Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
v). Elimu Sekondari
vi). Maendeleo ya Jamii
vii). Kilimo, Mifugo na Uvuvi
viii). Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
ix). Mipango na Uratibu
i). Usimamizi wa Taka na Usafi
ii). Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
iii). Michezo, Utamaduni na Sanaa
iv). Fedha na Uhasibu
v). Huduma za Sheria
vi). Ukaguzi wa Ndani
vii). Usimamizi wa Ununuzi
viii). TEHAMA
ix). Mawasiliano Serikalini
Mwenyekiti wa Halmashauri ni Kiongozi Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ni Mtendaji Mkuu upande wa Serikali za Mitaa.
Wilaya inaongozwa na BARAZA LA MADIWANI lenye wajumbe 51 kati yao 2 ni wabunge wa kuchaguliwa kwa mchanganuo ufuatao:-
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.