Lengo
Kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo ya viwanda, biashara, masoko na uwekezaji.
Majukumu Kitengo kitafanya kazi zifuatazo:-
• Kuratibu utekelezaji wa sera, sheria, kanuni na taratibu zinazohusiana na viwanda, biashara, masoko na uwekezaji;
• Kukuza viwanda, biashara, masoko na uwekezaji katika Halmashauri;
• Kupanga na kuendeleza maeneo ya viwanda na hifadhi kwa kushirikiana na wadau wengine wakuu;
• Kupanga vivutio vya viwanda, biashara, masoko na kukuza uwekezaji;
• Kukuza maendeleo ya Biashara Ndogo na za Kati (SMEs);
• Kuendeleza mapendekezo na miradi ya uwekezaji;
• Kuendeleza hatua za maendeleo ya sekta binafsi;
• Kuanzisha na kusimamia kanzidata ya viwanda, biashara, masoko na uwekezaji;
• Kusimamia usimamizi wa kituo kimoja cha biashara;
• Kufanya utafiti wa kukuza uwekezaji;
• Kuratibu Jukwaa la Biashara;
• Kusimamia shughuli za minada na masoko katika Halmashauri;
• Kutekeleza Mkakati wa Maendeleo ya Biashara kwa wafanyabiashara wadogo na watoa huduma; na
• Kuweka Mazingira bora ya Biashara na uwekezaji ili kukuza Biashara na Uwekezaji.
Divisheni hii ina Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:-
• Sehemu ya Maendeleo ya Viwanda na Uwekezaji; na
• Sehemu ya Biashara na Masoko.
Sehemu ya Maendeleo ya Viwanda na Uwekezaji
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:-
• Kuratibu utekelezaji wa sera, sheria, kanuni na taratibu za sekta ya viwanda na uwekezaji;
• Kukuza na kuratibu utekelezaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi;
• Kutenga, kuendeleza na kufuatilia maeneo ya viwanda na hifadhi;
• Kutoa ushauri kuhusu uboreshaji wa sera za Viwanda na kuratibu mikutano ya kisekta;
• Kukuza uzalishaji wa malighafi mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya viwandani;
• Kutayarisha na kutunza rejista za viwanda na vitega uchumi;
• Kupanga na kukadiria ushuru kwa viwanda vidogo;
• Kuendeleza na kupitia upya wasifu wa uwekezaji;
• Kukuza uwekezaji wa sekta binafsi;
• Kuratibu na kutoa ushauri kwa wawekezaji; na
• Kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Sehemu ya Biashara na Masoko
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo; -
• Kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, kanuni na taratibu za biashara na masoko;
• Kutoa ujuzi wa ujasiriamali kwa jumuiya ya wafanyabiashara;
• Kuratibu na kutoa ushauri kuhusu shughuli za usajili wa biashara;
• Kuchambua taarifa za biashara na masoko na ushauri ipasavyo;
• Kuratibu kongamano la Baraza la Biashara la Wilaya;
• Kukuza ubia wa sekta binafsi ya umma;
• Kusimamia shughuli za minada na masoko katika Halmashauri; na
• Kukusanya na kusambaza taarifa za masoko ya bidhaa na huduma kwa wahusika;
• Kutekeleza Mkakati wa Kukuza Biashara kwa wachuuzi wadogo na watoa huduma za biashara ndogo ndogo; na
• Kuweka Mazingira Bora ya Biashara.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.