Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Vincent Naano leo Septemba 26, 2025 amekabidhi vitendea kazi kwa Watmishi wa Kada mbalimbali vilivyotolewa na Serikali ya awamu ya Sita kwa ajili ya kufanikisha utendaji kazi wao.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Vishikwambi 21 kwa ajili ya Utambuzi wa Mifugo na Chanjo, Kompyuta 20 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za Afya, Pikipiki 12 kwa ajili ya Maafisa Mifugo ngazi ya Kata, POS 11 kwa ajili ya kuksanyia mapato.
Waliokabidhiwa vifaa hivyo ni Maafisa Mifugo ngazi ya Kata kutoka katika Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Waganga wafawidhi wa Zahanati na Vituo vya Afya kutoka Divisheni ya Huduma za Afya, lishe na Ustawi wa Jamii na Wakusanya Mapato walio chini ya Kitengo cha Fedha.
Akiongea na Watumishi hao amewataka wakavitumie vema kama malengo ya Serikali yanavyotaka na kuvitunza ili kuleta tija.
Naye MKurugenzi Mtendaji amewataka Maafisa Mifugo kutumia pikipiki na vishikwambi kwa malengo yaliyokusudiwa, Waganga wafawidhi kutumia mfumo wa GOTHOMIS kwani hakuna kipingamizi cha vindea kazi,huku akiwaasa Wakusanya Mapato kutumia vema POS na kutozichezea.
Aidha Watumishi wamevipokea kwa furaha huku wakiahidi kwenda kuvitumia vema ili kutimiza hadhima njema ya Serikali na kutoa huduma kwa jamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.