Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu imezindua chanjo ya Mifugo kwa ajili ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya mapafu kwa Ng’ombe. Mifugo inayotarajiwa kuchanjwa ni Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo na Kuku.
Akizindua zoezi la chanjo hiyo, Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe Dkt Vicent Naano Anney amesema lazima zoezi hili linasimamiwe vyema ili mifugo yote ichanjwe kwani ni lazima wala siyo hiari.
Akisisitiza alisema “Zoezi la chanjo ya Mifugo siyo la hiari ni lazima maana lipo kisheria na linasaidia kupunguza magonjwa ya mlipo kwa mifugo hivyo Wafugaji wote muone umuhimu wa zoezi hili kwakuwapeleka mifugo wenu wakapate chanjo” Dc Maswa Dkt Vicent Anney
Pia amewashauri wafugaji kutafuta mbegu bora za mifugo ili kuleta ushindani katika soko la nyama nje ya nchi na kuongeza uchumi na tija kwa wafugaji huku akiagiza wataokaidi kuchanja mifugo yao wapelekwe Mahakamani kwa hatua za kisheria.
Naye Daktari wa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt Charles Msira ametaja idadi ya mifugo na malengo waliyojiwekea katika kufanikisha zoezi hilo la uchanjaji wa mifugo. Aidha Dkt Msira amesema kuwa chanjo hii ni Muhimu kwa mifugo kwani itaenda kudhibiti milipuko ya magonjwa ya mifugo, kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo yenye Ubora na Salama kwa watumiaji huku akitaja hasara za kutochanja mifugo.
Nao baadhi ya wafugaji wa Kata ya Nyabubinza wakaelezea furaha yao baada ya kuletewa huduma ya chanjo katika eneo lao huku wakilinganisha hapo awali walikuwa wanapoteza mifugo kutokana na magonjwa mbalimbali na kutumia fedha nyingi kutibu mifugo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.