Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Maswa limezinduliwa leo Tarehe 02/12/2025 ambapo Waheshimiwa Madiwani wameapa kiapo cha utii na cha maadili ya utumishi wa umma. Pia wamechagua uongozi yaani Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo Mheshimiwa Miza Marietha Jishuli Diwani mteule wa Kata ya Isanga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2025/2030 na Mheshimiwa Mary Misangu Saganda Diwani mteule wa Kata ya Sukuma amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Katika kikao hicho zimeundwa kamati za Kudumu za Halmashauri, Kamati nyingine na kuchagua viongozi wa Kamati hizo. Vilevile wamesomewa taarifa ya utekelezaji ya kipindi cha Julai hadi Novemba 2025 ambayo imeonyesha mafanikio mengi ikiwemo ujenzi wa Shule tatu mpya za Sekondari ambazo ni Bukigi Day, Isageng’e na Mwabaratulu, ununuzi wa Gari jipya kwa mapato ya ndani na miradi mingine mingi.
Akiongea na Waheshimiwa Madiwani wateule Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Vicent Naano Anney amewasihi Waheshimiwa Madiwani wakafanye kazi kwa ushirikiano na wataalamu, wakasimamie kusanyaji wa mapato na kubana mianya ya upotevu wa mapato. Pia amewasisitiza waepuke migongano ya kimaslahi katika utekelezaji wa majukumu yao ili isije sababisha migogoro isiyo ya lazima na wahudhurie vikao na kutoa maamuzi sahihi ya masuala mhimu ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Akiwasalimia wateule wenzake mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Dkt Lugomela ameahidi kufanya kazi Pamoja na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi na Waheshimiwa Madiwani wote kusukuma gurudumu la maeendeleo Wilayani Maswa.

Waheshimiwa Madiwani wakihapa leo tarehe 2/12/2025 wakati wa uzinduzi wa Baraza Jipya la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg Maisha Selemani Mtipa wa kwa Kulia akitoa mkono wa pongezi kwa Viongozi wateule, wa Katikati ni Mwenekiti Mteule Mhe. Miza Marietha Jishuli na wa kwanza Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe. Mary Misangu Saganda.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.