Lengo
Kutoa huduma bora za afya, ustawi wa jamii na lishe kwa ustawi wa jamii.
Majukumu ya Divisheni hii itafanya kazi zifuatazo:-
• Kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na taratibu za utoaji wa huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe;
• Kuandaa mipango na programu za muda mfupi na mrefu za sekta ya afya katika Halmashauri;
• Kukuza ushiriki wa wadau mbalimbali katika shughuli za afya, ustawi wa jamii na lishe;
• Kutayarisha na kuwasilisha taarifa za huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe kwa mamlaka husika;
• Kuandaa mikakati ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza;
• Kusimamia miradi ya afya, ustawi wa jamii na lishe; na
• Kusimamia kanzidata ya masuala ya afya, ustawi wa jamii na huduma za lishe.
Idara ina Sehemu tatu (3) kama ifuatavyo:-
• Sehemu ya Huduma za Afya;
• Sehemu ya Ustawi wa Jamii; na
• Sehemu ya Huduma za Lishe.
Sehemu ya Huduma za Afya
Sehemu hii inafanya shughuli zifuatazo:-
• Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, na Taratibu za huduma za afya;
• Kushauri kuhusu uratibu na kujenga uwezo wa huduma za afya;
• Kuandaa mipango na programu za muda mfupi na mrefu za huduma za afya;
• Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau kuhusu masuala ya huduma za afya; na
• Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya magonjwa ya mlipuko, kuzuia magonjwa yasiyoambukiza, ya kuambukiza na ibuka katika vituo vyote, jamii na sehemu za kuingilia.
Sehemu ya Ustawi wa Jamii
Sehemu hii inafanya shughuli zifuatazo:-
• Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na taratibu za uboreshaji wa ustawi wa jamii;
• Kuandaa mipango na miradi ya muda mfupi na mrefu ya Ustawi wa Jamii;
• Kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi ya ustawi wa jamii;
• Kuratibu na kusimamia miradi yote inayohusu Ustawi wa Jamii; na
• Kutayarisha taarifa zinazohusiana na ustawi wa jamii.
Sehemu ya Huduma za Lishe
Sehemu hii inafanya shughuli zifuatazo:-
• Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na taratibu za uboreshaji lishe;
• Kuandaa mipango na miradi ya muda mfupi na mrefu ya lishe;
• Kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi ya lishe;
• Kuratibu na kusimamia miradi yote inayohusu lishe;
• Kutayarisha taarifa zinazohusiana na lishe ya jamii;
• Kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya lishe;
• Kufuatilia na kutathmini utoaji wa huduma za lishe katika Halmashauri;
• Kukusanya na kuchambua taarifa za huduma za lishe; na
• Kutoa huduma za lishe kwa watoto, watu wazima na watu wenye mahitaji maalum.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.