Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg Maisha. S. Mtipa leo tarehe 02.02.2026 amekabidhi vifaa saidizi vya kidigitali kompyuta mbili( Laptops ) kwa walimu wenye mahitaji maalumu kwa lengo la kurahisisha ufundishaji kwa walimu hao.
Vifaa hivyo vimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo Walimu walionufaika na vifaa hivyo ni Mwalimu John Lucas Ketegwe kutoka Shule ya Sekondari ya wasichana Maswa pamoja na Mwalimu Mzee Luchagula kutoka Shule ya Sekondari Binza.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi Mtendaji ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Dk.t Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kutoa vifaa kwa walimu hao ili viweze kuboresha shughuli za kazi zao.
Aidha Ndg. Mtipa ametoa wito kwa Afisa Mipango, Afisa Elimu Sekondari na Afisa Elimu Msingi kuwabaini walimu wote wenye mahitaji maalumu ili watengewe bajeti kwa lengo la kuwasadia kununua vyombo vya usafiri kwa lengo la kufika kazini kwa wakati na kufanya kazi ili waone ni kwa namna gani serikali inathamini mchango wao.
“Tunaishukuru serikali lakini serikali ndio sisi na tunatakiwa tuweke mipango kwa hiyo tunatakiwa tufanye katika mipango yetu ya bajeti tuweke kipaumbele kwa ajili yao, niwapongeze sana walimu hivyo vifaa mlivyovipata mkavitumie katika kazi zenu kwa kuwa serikali imeona umuhimu wa kuwapa vifaa na nyinyi mkaisemee serikali”. Amesema Mkurugenzi Mtendaji
Nao Walimu wameishukuru serikali, Mkurugenzi Mtendaji, Viongozi wa Mkoa na Wilaya, Idara ya Elimu sekondari kwa kuendelea kuwajali na kuhakikisha wanapata mazingira mazuri ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kuwa bega kwa bega kutatua changamoto zao na pia wamemuomba Mkurugenzi Mtendaji kuharakisha mpango wa usafiri ili kuwasaidia kufika kazini kwa wakati hasahasa kipindi cha mvua.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Maisha Seleman Mtipa (Kulia) akimkabidhi "Laptop" Mwl. Mzee Luchagula

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Maisha Seleman Mtipa (kulia) akimkabidhi "Laptop" Mwl. John Lucas Ketegwe
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.