Idara ilianza mwaka 2009 ikiwa na jumla ya shule za Sekondari za serikali 36 kati ya shule hizi shule 4 zikiwa mjini na 32 ziko vijijini na shule za watu binafsi mbili. Kwa sasa kuna shule za sekondari 40 ambapo 36 ni za serikali na 4 za binafsi. Kuna Maofisa 3 upande wa utawala (Afisa Elimu Sekondari Mwl Joseph Mashauri, Afisa Elimu Taaluma Mwl. Mwajuma Likindi na Afisa Vifaa na Takwimu Mwl. Elias H. Mbiji).
Kusimamia ufundishaji na uendeshaji wa shule 40 za sekondari
1.Kusimamia ujenzi wa miundombinu yote ya sekondari ikiwemo ujenzi wa maabara
2.Kusimamia uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza
3.Kusimamia usajili wa wanafunzi wanaofanya mtihani wa kidato cha pili, nne, sita na chuo cha walimu kila mwaka wa masomo
4.Kusimamia uendeshaji wa mashindano ya UMISETA ngazi ya wilaya
5.Kupanga walimu wapya wanaolipoti kwenye Halmashauri yetu kila mwaka
6.Kugawa na kupeleka vitabu, ruzuku ya uendeshaji na vifaa vingine vya kufundishia katika shule zote 36 za serikali
7.Kusimamia uendeshaji wa mitihani mbalimbali ya kitaifa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.