Idara ya Utawala na Utumishi ni nguzo kuu katika kuhakikisha uwajibikaji na utekelezaji wa shughuli mbalimbali ili kufikia dira na malengo ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Maswa. Ikiwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali watu yenye weledi, uwezo na mtawanyiko sawia katika maeneo mbalimbali ya kiutawala ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa. Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina idadi ya Tarafa 3 ambazo ni Mwagala, Nung’hu na Sengerema. Kata 36 ambazoni Binza, Nyalikungu, Zanzui, Sukuma, Ng’wigwa, Masela, Kadoto, Nguliguli, Ipililo, Seng’wa, Senani, Buchambi, Mwamashimba, Budekwa, Mwang’honoli, Badi, Malampaka, Lalago, Dakama, Isanga, Jija, Kulimi, Shishiyu, Nyabubinza, Sola, Shanwa, Mbalagane, Bugarama, Mwabayanda, Busangi Mpindo, Mataba, Mwabaratulu, Sangamwalugesha, Mwamanenge, Busilili na vijiji 120. Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina jumla ya watumishi 2609 katika idara 12 za Utawala na Utumishi, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Afya, Mipango Kilimo Umwagiliaji na Ushirika, Mifugo na Nyuki, Maendeleo ya Jamii, Ardhi, Fedha, Maji na Ujenzi na vitengo sita (6) ambavyo ni Kitengo cha Manunuzi, Sheria, Mkaguzi wa Ndani, Uchaguzi, Nyuki na Tehama.
Shughuli Zinazofanyika
Shughuli kuu zinazofanyika katika idara ya utawala na utumishi ni pamoja na kuajiri, kupandisha madaraja, kusimamia masuala ya kinidhamu ya watumishi , kuunda bajeti ya utumishi (kusimamia ikama ya watumishi) , usafishaji wa taarifa za kiutumishi, kutatua kero na malalamiko ya watumishi ikiwa ni pamoja na madai yao, kusimamia malipo na makato mbalimbali katika mishahara ya watumishi.
Mafanikio
Mafanikio yalipatikana katika idara ya Utawala na Utumishi ni kama vile kupunguza kero na malalamiko ya watumishi kwa kiasi kikubwa ikiwa ni zao la usimamizi wa misingi ya utawala bora katika Utumishi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Changamoto
Pamoja na mafanikio vilevile Idara ya Utawala na Utumishi inakabiliana na changamoto zifuatazo ni baadhi ya watumishi kutozingatia sheria, kanuni na taratibu, kasi ya upatikanaji wa watumishi ni ndogo hususani kada ya afya na madai ya watumishi kutolipwa kwa wakati muafaka,Kukosekana kwa ofisi na nyumba za watumishi za kutosha katika vituo vya kazi.
Matarajio
Idara ya Utawala na Utumishi inatarajia kuwekeza katika kujenga mazingira rafiki ya kazi kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kutatua kero na malalamiko yao kwa wakati,kuongeza idadi ya ofisi na makazi ya watumishi katika ngazi ya kata na vijiji.Kuongeza ufanisi na uwajibikaji wa watumishi ili kutoa huduma bora . Vile vile inalenga katika kuhakikisha mtawanyiko sahihi wa watumishi katika maeneo mbalimbali ya kiutawala ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.