Idara ya maendeleo ya Jamii ina vitengo vitano ambavyo ni :
i.Kitengo cha utafiti takwimu na mipango.
ii.Kitengo cha wanawake na watoto
iii.Kitengo cha kikosi cha ujenzi
iv.Kitengo cha kudhibiti Ukimwi
v.Kitengo cha vijana
Kitengo cha utafiti takwimu na mipango
Shughuli zinazofanyika ni;
a.Uhamasishaji wa shughuli za kujitegemea ambazo ni pamoja na;
-Ujenzi wa madarasa, Zahanati, Vituo vya afya, na nyumba za walimu
-kushiriki katika utengenezaji wa barabara na uchimbaji wa visima.
b.Ukusanyaji wa takwimu mbalimbali, mfano;
-Takwimu za watu wenye ulemavu
-Takwimu za vikundi
-Takwimu za ujenzi wa nyumba bora
-Takwimu za watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
-Takwimu za vituo vya kulelea watoto wadogo mchana
-Takwimu za wazee
c.Kusaidia vikundi kuandika maandiko ya miradi
d.Kusaidia kuelekeza jamii katika upangaji mipango ya maendeleo.
e.Kuwezesha jamii kutambua matatizo waliyonayo na hivyo kuyapanga kulingana na umuhimu wake kisha kuyatatua kwa kutumia fursa na rasmali walizonazo.
f.Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera za Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto.
g.Kusimamia utafiti kuhusu matatizo mbalimbali katika jamii.
h.Kutambua azaki zilizomo katika wilaya na kuratibu shughuli zake.
Kitengo cha wanawake na watoto
Shughuli zinazofanyika ni;
i.Utoaji wa elimu ya ujasiliamali kwa vikundi vya wanawake.
ii.Kuelimisha jamii juu ya athari ya mila na desturi potofu zinazogandamiza wanawake na watoto.
iii.Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
iv.Kutembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
v.Kufanya ufuatiliaji na kutoa ushauri kwa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
vi.Kuelimisha jamii katika masuala mazima ya usawa wa kijinsia.
vii.Uundaji wa vikundi vya wanawake vya kiuchumi.
viii.Kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake.
ix.Kutoa vifaa vya michezo na vya kujifunzia kwa watoto wa chekechea
Kitengo cha vijana
Kitengo cha vijana kinafanya kazi zifuatazo;
a.Utoaji wa elimu ya ujasiliamali kwa vikundi vya vijana.
b.Kuelimisha vijana juu ya umuhimu wa kuunda vikundi na kufanya kazi zao katika vikundi
c.Kufanya ufuatiliaji na kutoa ushauri kwa vikundi vya vijana
d.Uundaji wa vikundi vya vijana vya vya kiuchumi
e.Kutoa mikopo kwa vijana.kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini.
f.Kutoa vifaa / baiskeli kwa watu wenye
Kitengo kikosi cha ujenzi
Shughuli zinazofanyika
i.Kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali kupitia fani za ufundi kama vile ufundi Mwashi, Uselemala , uhunzi na uchomeleaji.
ii.Kutoa mafunzo kwa vikundi vya mafundi kwa kushirikiana na taasisi zingine za serikali kama vile mamlaka ya ufundi stadi VETA.
iii.Kuibua na kusambaza teknolojia rahisi na sahihi zinazoweza kuisaidia jamii katika shughuli za kila siku kwa lengo la kujiletea maendeleo.
iv.Kushirikiana na kamati za miradi ya maendeleo kwenye ngazi ya kata na vijiji katika kusimamia shughuli za miradi ya maendeleo zinazotekelezwa na jamii.
v.Kutoa tafsiri ya teknolojia mpya juu ya matumizi yake mfano ujenzi wa nyumba bora na zenye gharama nafuu kwa kutumia matofari yanayotengenezwa kwa kutumia mashine za Cinvarumm Interlocking pamoja na Hydroform mashine.
vi.Kuhamasisha jamii ili iweze kujijengea makazi bora kwa maana ya nyumba za kuishi ikiwa ni pamoja na kutoa tafsiri ya nyumba bora kwa kutaja sifa zake ambazo ni ; nyumba bora imejengwa kwa kuzingatia sifa za majenzi , msingi uliojengwa kwa mawe au matofari , ukuta imara , madirisha yanayoingiza mwanga na hewa ya kutosha ndani, iliyo na jiko na choo pamoja na store sambamba na hayo lazima iwe na shimo la kutupia taka ngumu na laini.
vii.Kusimamia shughuli za miradi ya maendeleo zinazotekelezwa kwa kutumia nguvu za wananchi mfano ujenzi wa vyumba vya madarasa , vyoo na zahanati.
viii.Kutoa mwelekeo kwa vikundi vya ujasiliamali kuona kwamba uwezekano wa kujiletea maendeleo katika maeneo yao inawezekana kwa kutumia raslimali walizonazo kwenye maeneo yao na wataalamu waliopo.
Kitengo cha kudhibiti UKIMWI
Kitengo hiki kinajishughulisha na udhibiti wa V.V.U na UKIMWI. Lengo kuu ni kuboresha huduma za V.V.U na UKIMWI kuhamasisha na kuelimisha jamii kujikinga na maambukizi mapya ya V.V.U. Ili kufanikisha lengo , Wilaya haina budi kuungana na Serikali kuu kuunganisha nguvu za Serikali za Mitaa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na vikundi vya kijamii vikiwepo vya Watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI kushughulikia Afua ( Intervention) zifuatazo;
-Mazingira wezeshi
-Kinga
-Matunzo na matibabu
-Kupunguza athari za V.V.U na UKIMWI kwa jamii
Huduma za kijamii
i.Pamoja na shughuli zinazoratibiwa na Idara kupitia vitengo vyake pia huratibu shughuli na huduma za jamii kama ifuatavyo; Huduma za ibada katika madhehebu ya Kiislam, Katoliki,AEGT,FB Fellowship,
CALVARY,The Pool of Sloam, SABATO, AIC, FPCT, ANGLICAN, KKKT, PAG,TDG, OMEGA, KLAPT, MALAMPAKA na SAYUNI.
ii.Biashara mbalimbali kama vile biashara za mazao ya kilimo cha pamba, alizeti, mahindi, mpunga,viazi vitamu, choroko, kunde, dengu, karanga, njugu mawe, ufuta, mboga mboga na matunnda.
iii.Shughuli za ufugaji wa Ng’ombe, mbuzi, kondoo,nguruwe,nyuki,kuku, na bata.
iv.Shughuli za minada, magulio na masoko .
v.Kumbi za mikutano za Halmashauri ya wilaya , Ndemax na Millenium.
vi.Huduma za Mahakama 13 na magereza 2.
vii.Shughuli katika shule za awali 120, kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi (Dekapori), chuo cha maendeleo ya wananchi , kituo cha kulelea watoto wenye mtindio wa ubongo (Binza Primary), na jengo la shughuli za wananchi (SIDO).
viii.Huduma za kifedha katika taasisi za NMB, CRDB, POSTA, BAYPOT, VISION FUND na PRIDE.
ix.Huduma za mawasiliano katika taasisi za TTCL, AIRTEL, VODACOM, TIGO, ZANTEL,HALOTEL TANESCO NA REDIO SIBUKA
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.