Leo tarehe 10/11/2025 umefanyika uzinduzi wa jengo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Maswa lenye ghorofa moja. Shughuli hiyo imeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Vicent Naano Anney kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg; Maisha Seleman Mtipa. Katika shughuli hiyo wameshiriki wadau mbalimbali wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Maswa, Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Viongozi wa Dini, Watumishi wa Halmashauri, Viongozi wa Tiba Asili, Wazee maarufu, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa vyama vya siasa na wageni mbalimbali waalikwa.
Ili kuanza kazi Viongozi wa Dini wameombea Amani na kisha kuwashauri watumishi wafanye kazi kwa Weledi na Amani.
Akitoa taarifa ya Utekelezaji Afisa Mipango Wilaya Ndg; Julius Ikongora John amesema mradi ulianza utekeleza mnamo tarehe 23/09/2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30/12/2025. Aidha fedha zilizopokelewa zilizopokelewa kwa ajili ya mradi huu ni Tsh. 3,300,000,000/= na mradi hadi sasa umefikia Zaidi ya asilimia 90 ya utekelezaji.
Mgeni rasmi yaani Mkuu wa Wilaya ya Maswa akiongea na hadhara, ameiongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi Mtendaji, Timu ya Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa usimamizi mzuri na kufanikisha ujenzi wa jengo hili. Amehimiza mshikamano kwa watu wote ili kazi zifanyike kwa amani na uadilifu. Pia amewaomba wafanyabiashara kutumia fursa iliyopo kuendeleza maeneo yaliyopo katika Ofisi hii ili huduma na mahitaji mhimu yapatikane.
Zoezi la uzinduzi limeambatana na upandaji wa miti katika eneo la Ofisi hii.

Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.