Leo tarehe 21/12/2021 Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Maswa.
Miradi iliyokaguliwa ni ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa iliyofadhiliwa na IMF, Mradi wa Maji na Ujenzi wa Mitaro ya kupitisha maji katika Barabara za mjini Maswa.
Kamati hiyo imekagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule za Sekondari tano ambazo ni Malampaka vyumba viwili, Isanga vyumba viwili, Nyalikungu vyumba viwili, Mwakaleka vyumba viwili, Binza vyumba vitatu na Zanzui chumba kimoja. Ujenzi huo uko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Kamati imetoa pongezi kwa wasimamizi na wanaofanya kazi hiyo kuwa kazi ni nzuri. Pia wametoa maagizo kazi kufanyika haraka ili ikamilike na kukabidhiwa kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.