Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira imafanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halamashauri ya Wilay ya Maswa. Kamati hiyo imetembelea mradi wa Ukarabati wa Soko kuu la Maswa lililoko mjini Maswa Kata ya Sola, Mradi wa Vibanda vya Stendi Mpya Kata ya Shanwa, Ukaguzi wa maendeleo ya zoezi la chanjo ya mifugo katika Kijiji cha Nguliguli Kata ya Nguliguli na kukagua shughuli za Kikundi cha REK AGRIFARM kilichoko katika Kijiji cha Mwabayanda Kata ya Ng'wigwa.
Katika mradi wa soko, limejengwa jengo pamoja na meza 33 ambapo mradi uko hatua ya mwsiho kukamilika tayari kuanza kazi. Mradi wa vibanda zaidi ya 300 vilivyoko stendi mpya, wajumbe wamesisitiza zifanyike juhudi za ziada kukamilisha miundo mbinu mingine ili wananchi waweze kuvitumia. Katika zoezi la chanjo wamesifu uwepo wake katika Wilaya yetu, mtaalam anayechanja akaomba taarifa zitolewe kwa wakati katika Kata zilizobakia ili wafugaji walete mifugo yao yote kwa wakati. Kikundi cha REK AGRIFARM kimepata Mkopo wa Sh. 4,000,000/= kutoka Halmashauri na kuanzisha shughuli ya ufugaji wa Kuku wa Mayai, hadi sasa wana kuku 180 ambapo wanatarajia kuanza uzalishaji mwezi ujao.
Wajumbe wa kamati hii wamesifu shughuli zinazotekelezwa na kusisitiza penye changamoto ziwaslishwe sehemu husika mapema na kufanyiwa kazi ili maendeleo ya wananchi yasikwame.
Muonekano wa Soko kwa nje
Muonekano wa Meza za Sokoni
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.