• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Zahanati ya Mwabayanda “M” yazinduliwa

Posted on: April 27th, 2023

Kijiji cha Mwabayanda ni miongoni mwa vijiji vinavyounda Kata ya Ng’wigwa ambapo kwa muda mrefu hakikuwa na huduma ya afya hivyo kupelekea wananchi wake kutembea umbali mrefu wa  kilometa 15 kwenda kijiji cha Igongwa au Hospitali ya Wilaya ya Maswa kupata huduma.

Serikali ya kijiji hicho cha Mwabayanda kwa kushirikiana na wananchi walijenga boma la Zahanati hiyo ambapo serikali ya Mhe. Dkt  Samia Suluhu Hassan katika kuunga mkono jitihada za wanachi hao ilitoa shilingi milioni hamsini kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi Ndg. Marko Nkwimba ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kupeleka fedha katika kijiji hicho ambayo imesaidia wananchi hao kuanza kupata huduma mbalimbali za kiafya  katika zahanati hiyo.

Pia Ndg Nkwimba aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano waliouonesha kwa kujitolea nguvu kazi mpaka Zahanati hiyo ikakamilika. Pia aliwataka waache tabia zisizo nzuri za mila potofu ambazo zitasababisha mtumishi huyo kushindwa kukaa hapo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt Adorat Mpollo alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi milioni mia mbili kwa ajili ya kukamilisha maboma manne ikiwemo zahanati ya Mwabayanda “M” ambayo ilipata shilingi milioni hamsini kwa ajili ya kukamilisha zahanati hiyo pamoja na shilingi milioni hamsini na tano kwa ajili ya nyumba ya mtumishi ambazo zilitoka katika mfuko wa TASAF.

Aidha alimshukuru Mhe. Diwani wa Kata ya Ng’wigwa kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa  katika Kata yake pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji na timu yake kwa kusimamia vizuri mradi wa  zahanati hiyo mpaka ikakamilika na kuanza  kutoa huduma za kimatibabu.

“Tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao wote ambao wameuonyesha kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kutoa nguvu zao hili jengo mpaka lilipofikia kwa nguvu za wananchi sio jambo la kitoto, lakini pia kutoa nguvu zao katika ujenzi wa nyumba ya mtumishi”.

Mganga Mkuu wa Wilaya alitoa wito kwa akina mama wajawazito na watoto  kuwahi katika zahanati kwa kuwa huduma imesogezwa karibu ili kuepukana na vifo vinavyotokana na uzazi pia ametoa rai kwa akina mama kuacha tabia za kujifungulia nyumbani au kwa wataalamu wa mitaani.  

Dkt mpollo alieleza kuwa serikali inaendelea kuboresha sekta ya afya ambapo mwaka wa fedha wa 2023/2024 Hospitali ya Wilaya imewekewa bajeti ya shilingi milioni mia tisa kwa ajili ya ukarabati wa majengo katika Hospitali hiyo.

Kwa upande wao wanachi wameishukuru serikali kwa kuwasogezea huduma hiyo katika kijiji hicho na wameahidi ushirikiano kwa mtumishi wa zahanati hiyo na kuomba serikali iwaongezee watumishi wengine kwa kuwa wananchi ni wengi watakaoenda kupata huduma hapo.


Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.