Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ametembelea Miradi ya kimkakati ya ujenzi wa Kiwanda cha chaki na kiwanda cha Vifungashio vilivyoko eneo la Ng'hami. Pamoja na kutembelea miradi ya kimkakati amefanikiwa kukagua na kuona utekelezaji wa kiwanda cha Unga Lishe kilichoko katika kijiji cha Njiapanda Kata ya Isanga.
Ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Simiyu chini ya Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa na Jumanne Sagini Katibu Tawala wa Mkoa kuanzisha mkakati wa Wilaya moja bidhaa moja na hatimaye Wilaya zake kuanza utekelezaji. Ametoa pongezi za pekee kwa uongozi wa Wilaya ya Maswa kwa kutenga eneo maalum kwa ajili ya Viwanda. Pia ametoa pongezi kwa Wah. Wabunge na Madiwani kwa ushirikiano wao kuhusu kuendesha gurudumu vema na hatimaye kutekeleza hazima ya Serikali ya uchumi wa Viwanda.
Ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kuwasiliana na TILDO kuhusu suala la zima la kutumia bidhaa chakavu za plastiki kutengeneza nyingine ili kusaidia kuendeleza viwanda vyetu.
Amemtaka Mkandarasi ( SUMA JKT) kazi ifanyike haraka ili kiwanda kianze kazi mapema. Mkandarasi amesema vifaa vimegizwa mara vitakavyowasili ndani ya Wiki tatu atakuwa amekamilisha kazi ya ujenzi.
Kutokana na udhubutu wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kutekeleza hazima ya Ujenzi wa Viwanda, Mhe. Bashungwa amesema "Nitakavyokuwa ninaongea Wilaya moja bidhaa moja, Wilaya ya Maswa itakuwa mfano kwa ujenzi wa Viwanda".
Aidha amejifunza kutoka Maswa, huko jimboni kwake Karagwe kuna zao kubwa la migomba wanavuna ndizi na kutengeneza pombe aina ya Lubisi ili mwakani waanze wao pia Wilaya moja bidhaa moja.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.