Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuona utekelezaji wa miradi hiyo ilipofikia.
Waziri Mkuu amezindua jengo la matibabu ya dharura katika hospitali ya Wilaya ya Maswa iliyopo Kata ya Sola ambalo limejengwa kwa shilingi milioni mia tatu 300.
Mhe. Waziri Mkuu akizindua Jengo la Matibabu ya Dharula katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa 26.03.2023
Mhe. Majaliwa alisisitita kuwa jengo hilo la matibabu ya dharura limejaa vifaa vya kisasa na linatoa huduma kwa wakazi wa Maswa na maeneo mengine kwa wagonjwa wote hasahasa kina mama wajawazito na madereva bodaboda waliopata ajali.
Mhe. Waziri Mkuu aliongeza kuwa wilaya ya Maswa ni wilaya ya kiuchumi na inasimamia na kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi katika wilaya zingine hivyo jengo hilo la dharura linapaswa kuwepo ili kutoa huduma kwa wananchi wote wa Maswa na mikoa mingine kwa kuwa barabara zimetengenezwa na wananchi wengi wanapita hapo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa TAMISEMI Dkt Festo Dugange alisema uboreshaji wa sekta ya afya unaendelea ambapo katika kipindi Cha miaka miwili serikali ya awamu ya sita imeleta watumishi, imejenga zahanati, vituo vya afya pamoja na majengo ya huduma za dharura katika mkoa wa Simiyu
Pia ameendelea kuwaasa wananchi wa Maswa kuwa hawana haja ya kukimbilia sehemu zingine kupata huduma ya dharura kwa kuwa serikali imesogeza huduma hiyo karibu ili kuwahudumia. Pia alisema vituo vyote vilivyojengwa vianze kutoa huduma na serikali ya awamu ya Sita italeta magari mawili kwa ajili ya kutoa huduma za wagonjwa na lingine kwa ajili ya kufanya huduma shirikishi.
Pia Waziri mkuu amekagua kiwanda Cha chaki kilichopo kitongoji cha Ng'hami katika Kata ya Nyalikungu ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 8 mpaka sasa na mkandarasi aliyetekeleza mradi huo ni Suma JKT na ameutaka uongozi wa halmashauri kusimamia kiwanda hicho ili kianze kuzalisha chaki na kutoa ajira na kuongza mapato ya serikali.
Mhe. Waziri Mkuu akipata maelezo namana kiwanda kinatakavyo fanya kazi za uzalishaji wa chaki
Mtambo wa kuchakata chaki katika Kiwanda cha Chaki Ng'hami Maswa
Mtambo wa kuchakata chaki katika Kiwanda cha Chaki Ng'hami Maswa
Sambamba na hayo pia amekagua ujenzi wa reli ya kisasa awamu ya tano kipande cha kutoka Isaka mpaka Mwanza chenye urefu wa KM 341 ambapo gharama ya ujenzi huo ni Dora bilioni 1.326 sawa na shilingi tilioni 3.062 mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 28.05 na wafanyakazi zaidi ya 6721 ni watanzania wakati Simiyu peke yake ikiwa na vijana zaidi ya 520 waliopata ajira katika mradi huo.
Mhe. Waziri Mkuu akikagua ujenzi wa Reli ya mwendo kasi kipande cha Isaka Mwanza katika eneo la Malampaka 26.03.2023
Akizungumza katika nyakati tofauti waziri Mkuu amesema serikali ya awamu ya sita inaendelea kutekeleza maelekezo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwaletea wananchi maendeleo, kusikiliza kero na kuzitatua.
“Nataka niwahakikishie tutafanya kazi ya kumsaidia Rais wetu usiku na mchana, wakati wa jua na mvua kali, hiyo ndio dhamira yetu ili tuweze kuwafikisha mahali pazuri"
Mhe Kassim Majaliwa amesema watumishi wa Halmashauri wanatakiwa kuongeza Kasi katika utoaji wa huduma kwa kuwafikia wananchi, kusikiliza kero zao pamoja na kutatua changamoto za wananchi
Aidha waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa Halmashauri kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa hizo kwa kuwa kituo kikubwa Cha reli kitavutia wananchi wengi kujenga pia amesema fursa zinakuja katika mradi huo, hivyo amewataka wananchi kuwekeza katika hoteli na gesti.
Kujenga eneo kubwa la kuweka maroli ili kuongeza ajira katika eneo hilo kwa sababu kituo hicho ni kikubwa ambacho kitahusisha kubeba na kushusha mizigo kwa kuwa reli hiyo ni ya kimataifa hivyo tatizo la usafiri litakuwa historia pia amewataka Halmashauri kupima maeneo yanayozunguka eneo hilo ili waweze kupatiwa maeneo yaliyopimwa ili wawe na hati miliki.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.