• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Waziri apongeza watumishi wa Afya Maswa kwa kutoa huduma nzuri

Posted on: July 12th, 2023

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu yenye lengo la kufuatilia utoaji wa huduma za afya katika ngazi mbalimbali na kuhimiza watumishi wa afya kuzingatia weredi, maadili na viapo vyao katika utoaji wa huduma za afya.

Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo wakati akiongea na watumishi wa afya katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa wakati akitembelea na kukagua huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo ambapo amewapongeza watumishi kwa kutoa huduma nzuri.

Amesema serikali inatambua changamoto ya uhaba wa watumishi wa afya, hivyo amewataka watumishi kuwahudumia wananchi kwa weredi wakati serikali ikiendelea kuongeza watumishi wa sekta hiyo  na kuboresha  miundombinu yote ya afya kwa kuimalisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Pia Waziri wa Afya amesema serikali imeweka Mazingira mazuri kwa watumishi ili waweze kufanya kazi zao vizuri kwa kuwa serikali imetenga bajeti  kubwa  ambapo Wilaya ya Maswa imeongezewa bajeti kutoka Shilingi milioni 244 hadi shilingi bilioni 1.9 katika sekta ya afya.

Pia Mhe. Mwalimu ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kuboresha huduma za afya katika utoaji wa chanjo za polio, UVIKO-19 pamoja na chanjo zingine ambazo zimepunguza sana vifo vya watoto walio na umri chini ya  miaka mitano.

Aidha Waziri wa Afya ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kuajiri watumishi wa afya 65 kwa mkataba kupitia Fedha za mapato ya ndani na amewataka waendelee kufanya hivyo ili kuwasaidia wataalamu katika utoaji wa huduma za afya kwa lengo la kuokoa  maisha ya wananchi wa Maswa.

Vilevile Mhe. Mwalimu amewashukuru wadau wa maendeleo Mkapa Foundation na AMREF kwa kuajiri watumishi 36 ambao  wameisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa watumishi sambamba na hilo ametoa kongole kwa  Wilaya kwa kuwa  Hospitali ya wilaya, Zahanati na vituo vingi vya afya vimefungwa mfumo wa GOT HOMIS ambao utasaidia  ukusanyaji wa mapato.

Akiwa wilayani Maswa Waziri wa Afya ametembelea na kukagua jengo la huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa kuona huduma zinavyotolewa na wataalamu, ametembelea Chuo cha Maafisa tabibu na kuzungumza na watumishi pamoja na wanachuo, ametembelea jengo la watoto njiti na kuona namna ambavyo wanapatiwa huduma pamoja na Zahanati ya barikiwa iliyoko Kata ya Shanwa.


Matangazo

  • TANGAZO LA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI June 19, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WALIMU WA AWALI WAPATIWA MAFUNZO YA MBINU BORA ZA KUFUNDISHIA

    June 10, 2025
  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.