Kaimu Mkuu Wa Mkoa Wa Simiyu Mhe Anna Kidarya ameishukuru serikali kwa kupandisha madaraja na vyeo kwa watumishi katika mwaka wa fedha 2022|2023 ambapo watumishi waliopandishwa walikuwa 4585 Mkoani Simiyu.
“sisi wafanyakazi wa Mkoa wa Simiyu tunampongeza Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya katika kumuunga mkono sisi watumishi, viongozi wa serikali na umma kwa ujumla tunalo jukumu kubwa la kutatua kero mbalimbali za wananchi na watumishi zilizopo ndani ya uwezo wetu” Mhe Gidarya
Mhe Gidarya ameeleza hayo katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani MeiMosi yaliyofanyika tarehe 01 Mei 2024 katika uwanja wa CCM Bariadi Mji Mkoani Simiyu yenye kauli mbiu “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga ya Hali Ngumu ya Maisha”
Halmashauri zetu zinaendeshwa na mapato ya ndani kwa asilimia 80%, asilimia 20% tunategemea fedha za kutoka serikali kuu na wafadhiri twendeni tukaboreshe mapato ili tuweze kuondoa hizi changamoto ambazo ni za uwezo wa halmashauri zetu tukakusanye mapato tuhakikishe kwamba mapato haya yanawekwa katika mfumo ulioelekezwa kisheria ili sasa na sisi tuone mafanikio na halmashauri zetu.
kupitia maadhimisho hayo ya siku ya meimosi Mhe Gidarya ametoa maagizo kwa wakurugenzi kuhakikisha wanawalipa watumishi stahiki zao, ofisi ya utumishi kutoa huduma nzuri pamoja na watumishi kuepukana na mikopo umiza ambayo inasababisha kutokutimiza majukumu yao.
Pia Kaimu Mkuu wa Mkoa amewataka Wakuu wa Wilaya kuwa walezi katika wilaya ili kuleta ustawi kwa watumishi wote kuanzia ngazi ya chini na kutatua changamoto za watumishi ili kuboresha huduma katika mkoa wa simiyu.
Nae Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Ndg. Prisca Kayombo amewataka watumishi wa mkoa wa Simiyu kufanya kazi kwa kufata sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika sehemu za kazi kwa kuwa jukumu kubwa la mwajiri kwa mwajiriwa ni kumpatia maslahi bora.
Pia Katibu Tawala amesema Mhe Rais pia ameendelea kuboresha mazingira rafiki ya kufanyia kazi kwa kuweka miundombinu mizuri ya kufanyia kazi ikiwepo magari, madarasa, ofisi na vifaa vya TEHAMA pamoja na kuendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watumishi.
Katika maadhimisho hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa alikabidhi zawadi mbalimbai na vyeti kwa wafanyakazi bora kutoka katika taasisi mbalimbali za Mkoa wa Simiyu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.