Wasimamizi wa Vituo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wamepatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya usimamizi wa vituo vya kupigia kura wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Ndg Maisha Mtipa katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Binza Sekondari pamoja na shule ya wasichana Maswa leo tarehe 23.11.2024
Akizungumza na wasimamizi hao, Msimamizi wa Uchaguzi amewakumbusha kuzingatia Sheria, Miongozo na Kanuni, pia kufanya kazi kwa uadilifu, ufanisi, weredi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo la Kitaifa.
Pia amewathibitishia kuwa Serikali ya Wilaya itahakikisha kuwa usalama unaimarishwa katika kipindi chote cha uchaguzi ili zoezi hilo lifanyike kwa ufanisi mkubwa.
Aidha Ndg Mtipa amewataka wasimamizi hao kuwa makini katika zoezi hilo kwa kuwa serikali imetumia gharama kubwa katika kufanikisha Uchaguzi huo.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Maswa Mhe. Ramadhan Mhoja Shija amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa kuzingatia viapo walivyoviapa vya utii na uadilifu pamoja na kutunza siri katika jukumu hilo la kitaifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.