Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia kupitia wakala wa maendeleo ya uongozi wa Elimu ADEM imetoa mafuzo ya jumuiya za kujifunza kwa walimu wakuu 135 kutoka shule 135 za Wilaya ya Maswa na Maafisa Elimu Kata 36 yenye lengo la kujua mbinu mbalimbali za kutatua changamoto na kuongeza ufanisi katika majukumu yao.
Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku 4 katika shule ya msingi Shanwa iliyopo Kata ya sola kupitia mradi wa Shule Bora ulifadhiliwa na serikali ya uingereza kupitia mfuko wa UKaid.
Ester Marwa Mratibu wa mradi wa Shule Bora Mkoa wa Simiyu alitoa wito kwa Maafisa Elimu Kata na Walimu wakuu kuhusu mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kuboresha mbinu za uongozi na kiutawala katika ngazi zao za shule na Kata kwa kushirikiana, kuboresha mawasiliano na kutumia lugha nzuri za kiuongozi katika kutoa taarifa ili zilete motisha kwa walimu.
Pia aliongeza kuwa mafunzo yamelenga kuanzisha jumuiya kulingana na jeografia za maeneo Yao ambazo zitawasaidia kukutana mara kwa mara ili kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu mpya zitakazowawezesha kushirikiana na kutatua changamoto mbalimbali ili kuleta ufaulu kwa wanafunzi.
"Tunaamini kupitia mafunzo haya yatakuwa ni mwendelezo kwa sababu watakuwa wakikutana katika jumuiya hizi kubadilishana uzoefu na hadithi za mafanikio na Kila mmoja ataiga mazuri hivyo tutaboresha uongozi na walimu watafanya kazi kwa juhudi na kwa moyo na matokeo ya wanafunzi yatakwenda kuboreka sana kutokana na uongozi wa walimu hao". Alisema Mratibu wa Mkoa
Nae Richard Sungura Mkufunzi kutoka ADEM Mwanza alisema mafunzo hayo yanaenda kuleta mabadiliko makubwa Wilaya ya Maswa kwa kuwa viongozi wamebeba dhamana ya suluhisho la matatizo yote yanayowakabili walimu na wanafunzi.
" Kiongozi atapimwa kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na changamoto, ili uweze kuwa na ufanisi katika kukabiliana na changamoto jitathmini uone wapi umepungua na ujiimalishe na kiongozi hatakiwi kukata tamaa." Alisema mkufunzi Sungura
Afisa Elimu taaluma Wilaya ya Maswa Mwl Neema Makundi ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Shule Bora Wilaya aliwashukuru programu ya shule Bora na wawezeshaji mahiri kutoka ADEM kwa kuwawezesha walimu mambo mengi ambayo yatakwenda kuleta matokeo chanya katika usimamizi wa Elimu katika maeneo Yao.
Mwl Makundi alisema jumuiya za ufundishaji zitawasaidia kuwaweka pamoja kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika maeneo Yao ya kazi katika usimamizi wa Elimu na kutatua migogoro.
" Mafunzo haya yamekuja katika wakati muafaka kwa maana katika shule zetu changamoto ni nyingi ukisimama peke yako huwezi kufanya, lakini mnapokaa na mkashirikiana pamoja mna uwezo wa kufanya vizuri zaidi." Alisema mratibu wa mradi Wilaya
Kwa upande wake Mwl Emmanuel Makoye kutoka shule ya msingi Kakola aliishukuru progamu ya shule Bora kwa kuleta mafunzo hayo ya jumuiya za ujifuzaji kwa kuwa inaenda kuwa tiba ya kutatua migogoro kwa sababu jumuiya hizo zitaleta umoja na mshikamano baina yao
Mwl Ada Dizaya kutoka shule ya msingi Mkapa iliyopo Kata ya Kadoto alisema mafunzo hayo yamemjengea uwezo wa kwenda kufanya vizuri zaidi katika kituo chake Cha kazi na jamii inayonzunguka kwa sababu ataweza kutatua changamoto mbalimbali kwa sababu amejifunza mbinu mbalimbali kwa ufanisi.
"Mimi nafurahi sana kupata mafunzo haya, na mafunzo haya yaendelee ili kusudi yaweze kutusaidia na kutupa Elimu zaidi lengo kuu kuinua Elimu kama lengo lilivyokusudiwa." alisema mwl Dizaya
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.