Walimu wa shule za msingi Mkoa wa Simiyu wamepata mafunzo ya mbinu bora za ufundishaji yanayotolewa na mradi wa Elimu bora kuwasaidia walimu hao kumudu stadi za ufundishaji wa watoto wa darasa la Awali, darasa la Kwanza na darasa la Pili katika Kusoma, Kuhesabu na Kuandika (KKK).
Mafunzo hayo yanafanyika siku tano katika shule ya msingi Shanwa katika Halmashauri ya ya Wilaya ya Maswa ambapo walimu 120 kutoka shule 40 zinazofanyanyiwa majaribio na mradi huo wa Elimu bora zimeleta walimu watatu ambao wanafundisha madarasa ya awali, darasa la kwanza, na darasa la pili katika shule hizo kupata mafunzo.
Nae Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu William Mapunda amesema walimu hao wanaopata mafunzo hayo watatumika kufundisha walimu waliopo katika shule zingine kwenye Wilaya zao kwa kuwa wamepata mbinu nyingi mpya za namna ya kufundisha darasa lenye watoto wengi na tatizo la watoto kutokujua kusoma litakuwa limeisha kabisa.
"Malengo hapa hasa ya serikali ni kuhakikisha watoto hawa wanamudu stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu wakiwa bado kwenye madarasa ya chini kabla hawajafika madarasa ya juu hasa darasa la nne ambapo wataenda kufanyiwa upimaji wa namna walivyoweza kumudu hizo stadi" amesema Mapunda.
Kwa upande wake Afisa Mitahara kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania ambaye ni mratibu wa mafunzo ya mradi wa shule bora Ndg. Emmanuel Stanslaus amesema mafunzo hayo yamefanyika ikiwa bado kuna changamoto katika stadi hizo tatu za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) hivyo mradi unaendelea kutoa mafunzo hayo lengo likiwa ni kuwasaidia walimu wa madarasa hayo kuweza kumudu stadi za ufundishaji kwa watoto wa darasa la awali, darasa la kwanza na darasa la pili.
Katika hatua nyingine walimu wameishukuru serikali kupitia mradi wa shule bora kwa kuwaletea mafunzo hayo ambayo yamewasaidia kujua mbinu mbalimbali mpya ambazo watazitumia katika ufundishaji wao ili kuimarisha maarifa ambayo yatamsaidia mwanafunzi huyo wa darasa la awali, darasa la kwanza na darasa la pili kuelewa kwa haraka.
Pia walimu wamesema mafunzo hayo yamekuja wakati sahihi na kupitia mafunzo hayo walimu hao wamebaini mbinu ya kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu ambao watakuwepo katika madarasa wanayofundisha wito wao kwa serikali ni kuiomba iendelee kuleta mafunzo hayo ili yawajenge zaidi katika stadi hizo.
Mafunzo hayo pia yamelenga kuwashirikisha wazazi ambapo walimu wamefundishwa mada ambazo zitamuwezesha mzazi kushiriki katika kuboresha ufundishaji na wao kuwa sehemu ya kusaidia serikali kupata matokeo bora.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.