Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halamashauri ya Wilaya ya Maswa wamekagua ujenzi wa Kituo kipya cha Afya kinachojengwa katika Kijiji cha Ipililo Kata ya Ipililo.
Ujenzi wa Kituo hiki unajumuisha Majengo Matano ambayo ni Nyumba ya Mtumishi, Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), Jengo la Upasuaji, Jengo la Maabara na Jengo la Wodi ya Wazazi.
Ili kuanza utekelezaji wa mradi huu Serikali imetoa Kiasi cha Tsh. 400,000,000/=. Michango ya Wananchi inaendelea kuchangwa mabapo hadi sasa Tsh. 36,000,000/= zimeisha changwa.
Ujenzi umeishaanza uko katika hatua mbalimbali. Wakuu wa Idara wamewataka Mafundi kuongeza nguvu ili ujenzi ukamilike kwa wakati kulingana na Mikataba yao. Wamehimiza Kamati zote kushirikiana na kuwa mawasiliana ya mara kwa mara ili wasiwakwamishe mafundi katika hatua yoyote ile ya ujenzi.
Aidha Mtendaji wa Kata ya Ipililo pamoja na Mtendaji wa Kijiji cha Ipililo wameagizwa kuhakikisha rasilimali za ujenzi ( Kokoto na Mawe) zinafikishwa mapema iwezekanavyo ili kutokwamisha utekelezaji wa ujenzi.
Pia Watendaji kushirikiana na Kamati ya Ujenzi wahakikishe kesho Tarehe 11/08/2021 kazi ya ujenzi wa Wodi ya Wazazi uwe umeanza.
Muonekano wa Majengo uko katika hatua mbalimbali, zaidi soma MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA IPILILO.pdf
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.