Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Dkt Vincent Anney amewataka walimu kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili ikamilike kwa wakati ambapo ametoa wito kwa walimu wote wenye miradi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kuanzia tarehe 15 Aprili 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa amezungumza na walimu hao wakati wa mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa ununuzi wa umma kieletroniki (Nest) yaliyohusisha walimu wakuu wa shule za msingi, wakuu wa shule zote na maafisa manunuzi wa shule zote za msingi na sekondari Wilaya ya Maswa.
Pia amesema mafunzo hayo yatawasaidia kutatua changamoto mbalimbali za manunuzi walizokuwa wakizipata kabla ya mafunzo hayo na kuwawezesha kufanya vizuri baada ya kupata mafunzo hayo.
Pia amewasisitiza viongozi hao wanaosimamia miradi hiyo kuepukana na suala la wizi pamoja na miradi mibovu ambapo husababisha miradi hiyo kutokukamilika kwa ubora.
“Mimi nikikuta umeweka milango ya hovyo unatoa kwa gharama yako mwenyewe kwa sababu hela ya mama Samia haijapinda mimi nataka milango iliyonyooka, miradi iliyokamilika vizuri tukawasimamie mafundi.”
Pia ametoa wito kwa walimu hao kutimiza wajibu wao katika majukumu yao ili kuhakikisha wanafanya vizuri kitaaluma katika shule zao na amewataka kuanzisha vyanzo vingine vya mapato kama ujasiliamali ili kuepuka mikopo umiza.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.