Wataalamu kutoka PPRA Kanda ya ziwa wametoa mafunzo ya siku mbili ya matumizi ya mfumo wa manunuzi wa kierekroniki (NeST) kwa Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule, Walimu wa manunuzi wa shule za sekondari na msingi, Waganga Wafawidhi, Wataalamu wa manunuzi wa vituo vya kutola huduma za Afya, Watendaji wa Vijiji, Wadau wanaohusika na ununuzi ngazi ya kijiji, Maafisa Watendaji Kata, Wakuu wa Idara na Vitengo na Maafisa Ununuzi ngazi ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa lengo la kukuza uelewa na kuwajengea uwezo katika ununuzi wa umma.
Pia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kukidhi mahitaji na matarajio ya watumiaji, kurahisisha mchakato wa uombaji zabuni na kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya fedha kwenye ununuzi wa umma.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw. Robert Urassa ametoa shukrani kwa watalaamu kutoka PPRA kwa kuja kutoa mafunzo hayo kwa Watumiaji hao wa Mfumo kwa sababu yatawasaidia kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi ambapo kwa sasa masuala yote ya ununuzi lazima yapitie kwenye mfumo wa NeST.
“Kwa hiyo niwaombe sana ndugu washiriki tuweze kushiriki kwa ukamilifu na tuwe makini wakati wa mafunzo haya na ambapo utaona haujaelewa vizuri utauliza kwa sababu hii ni nafasi ambayo tumeipata kwa siku ya leo.” Amesema Bw. Urassa
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa tarehe 26.03.2025 hadi 27.03.2025
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.