Waandikishaji wa Wapiga Kura katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wamepata mafunzo maalumu yenye lengo la kwajengea uwezo katika zoezi la Uandikishaji wa wapiga kura litakalofanyika kuanzia tarehe 11 -20 Oktoba 2024 kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 27, Novemba 2024.
Akifungua mafunzo hayo Mwakilishi wa Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg Vivian Christian amewapongeza washiriki wote kwa kuteuliwa kutokana na ujuzi, uwezo na weredi walio nao. Ameeleza kila mmoja atapata elimu ya kutosha itakayomwezesha kutekeleza majukumu ili kufanikisha zoezi hilo.
Pia Ndg Vivian amesema mafunzo hayo yatahusisha namna bora ya ujazaji wa fomu, elimu ya uraia pamoja na kanuni na maadili ya Uchaguzi.
“Ni matumaini yangu kuwa mafunzo mtakayopata, natarajia mtafanya kazi kwa moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili la Kitaifa.” amesema Ndg Vivian
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.