Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amezindua rasmi leo zoezi la chanjo ya Mifugo Wilayani hapa. Akiongea na wafugaji waliofika katika eneo la Josho la kuoshea Mifugo Kijiji cha zanzui Kata ya Zanzui, Mkuu wa Wilaya amewahimiza Wananchi wote wanaofuga Ngómbe, Mbuzi na Kondoo kuleta Mifugo wao ili wachanjwe. Aidha amewataka viongozi wote wa Serikali na Siasa kushikiana kutoa hamasa kwa Wafugaji ili wapate elimu na kuelewa umhimu wa chanjo na pia kuhakikisha wanapeleka Mifugo yao katika maeneo ya kutolea chanjo tayari kwa kupata chanjo hiyo.
Akitoa taarifa ya zoezi hili Daktari wa Mifugo Wilaya ya Maswa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Maswa amesema zoezi limeanza kwa kufanya uhamasishaji kwa Viongozi wa jamii na wafugaji wenyewe kwa njia ya vikao, mikutano na matangazo mbalimbali. Aidha, Uchanjaji wa Ng’ombe dhidi ya Ugonjwa wa Mapafu kwa Ng’ombe na Sotoka ya Wanyama wadogo kwa Mbuzi na Kondoo umeanza katika maeneo mbalimbali tangu Tarehe 03.04.2023 na hadi sasa tumeshafanya zoezi hili katika Kata 8 ambapo jumla ya Ng’ombe 31,441, Mbuzi 3,483 na Kondoo 2,320 wameshachanjwa.
Pia Daktari wa Mifugo amesema "Kulingana na takwimu za Ng’ombe waliopigwa chapa mwaka 2017; Wilaya ya Maswa ina jumla ya Ng’ombe 305,640, Mbuzi 122,256 na Kondoo 76,410 na tunatarajia kuchanja angalau asilimia 80 ya wanyama hao katika vijiji vyote ili kukidhi vigezo vya kitaalamu katika udhibiti wa magonjwa na kwa mujibu wa Kanuni ya Chanjo na Uchanjaji Mifugo ya Mwaka 2020. Chanjo zote hizo zitatolewa kwa bei elekezi ya Serikali ya Tsh. 800/= kwa Ng’ombe na Tsh. 400/= kwa Mbuzi na Kondoo". Endapo Mfugaji atakaii kupeleka Mifugo kupata chanjo Daktari amesisitiza kwa kusema "Kwa mujibu wa sheria zilizopo endapo mtu atashindwa kuchanja mifugo yake atatozwa faini ya Tsh. 5,000/= kwa kila Ng’ombe na Tsh. 2,000 kwa Mbuzi na Kondoo au kushitakiwa, na endapo akipatikana na hatia anaweza kutozwa faini isiyopungua Tsh. 500,000/= na isiyozidi 10,000,000/= au kifungo jela kwa kipindi cha miezi 12 au vyote kwa pamoja kulingana na Kanuni ya Chanjo na Uchanjaji mifugo ya mwaka 2020."
Daktari wa Mifugo Wilaya ya Maswa akitoa taarifa ya zoezi la chanjo ya Mifugo kwa Mgeni rasmi leo 21/04/2023 katika eneo la Josho la kushea mifugo kijiji cha zanzui Kata ya Zanzui
Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa akiongea na Wafugaji wakati wa uzinuzi wa zoezi la chanjo ya Mifugo katika kijiji cha Zanzui 21/04/2023
Mkuu wa Wilaya akiongea na Wafugaji wakati wa uzinduzi wa zoezi la cjhanjo ya Mifugo katika kijiji cha Zanzui 21/04/2023
Mkuu wa Wilaya akikabidhi vifaa vya Chanjo kwa Daktari wa Mifugo 21/04/2023
Daktari wa Mifugo akichanja Ngómbe katika kijiji cha Zanzui 21/04/23
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.