Leo tarehe 24/12/2021 umefanyika uzinduzi wa upandaji miti Wilayani Maswa. Zoezi hilo limefanyika katika eneo la Shule ya Sekondari Zanzui iliyoko kata ya Zanzui ambapo miti 10,000 inatarajiwa kupandwa katika eneo hilo.
Mgeni Rasmi katika zoezi hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge. Walioshiriki katika kufanikisha zoezi hili ni Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Watumishi wa Halmashauri, Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanzui na Wananchi wa Kijiji cha Zanzui.
Akiongea na Wananchi na Wafanyakazi, Mkuu wa Wilaya ya Maswa amesema Wilaya ya Maswa ina lengo la kupanda Miti 1,500,000 katika kipindi cha Mwaka huu 2021/2022 hapa Zanzui tumeanza na zoezi hili litafanyika ndani ya siku 15 tangu sasa. Hivyo Taasisi zote na Wananchi wanahimizwa kupanda miti ili kuhifadhi mazingira yetu. Pia amesema mtu haruhusiwi kukata mti bila ruhusa ya mamlaka husika vinginevyo atakae kiuka utaratibu atachukuliwa hatua.
Amesisitiza pia Wananchi kulima zao la Pamba kwa kufuata kanuni na taratibu za kilimo bora.
Akihitimisha amewatakia wananchi woteheri ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.