Kambi maalumu la kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma katika shule za sekondari mkoani Simiyu limezinduliwa na kuanza rasmi terehe 3/4/2018. Kambi hili limezinduliwa na MKuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na linatarajiwa kufanya kazi kwa muda wa siku 10.
Akifungua kambi hiyo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani hapa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huu uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu.
Amesisitiza kwa kusema “Kama wanafunzi wetu wanakaa makambi ya michezo ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa nini wanafunzi hao hao wasikae kambi kwa ajili ya maendeleo ya taaluma; tukitaka kufanya mageuzi ya Mkoa huu ni lazima tuweke nguvu kwenye elimu, maeneo yenye uchumi mzuri wamewekeza sana kwenye elimu”
Lengo kuu la kambi hili ni kupitia mada zenye changamoto na kuwajengea uwezo wa kujiamini kufanya mtihani wa taifa wanaotarajia kuufanya hapo mwezi mei. Watoa mada ni walimu mahiri 40 wa masomo kutoka katika shule zenye kidato cha sita hapa Mkoani Simiyu.
Katika kambi hili Wanafunzi takribani 1000 wa kidato cha sita kutoka shule 11 wanatarajiwa kushiriki.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.