Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge amewaomba watendaji wa Kata kutoa elimu ya lishe kwa kuhamasisha wakuu wa shule kupeleka mahindi kusagwa katika mashine zenye virutubisho ambavyo vitasaidia watoto chini ya miaka mitano kuepukana na utapiamlo na udumavu.
Amesema virutubishi hivyo vya zinki, chuma, foliki asidi na vitamin B12 virutubishi hivi ni muhimu sana kwa afya ya watoto kwa ajili ya kuzuia utapiamlo mkali.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa Kata katika kikao cha kutathmini hali ya lishe ngazi ya Kata katika robo ya nne kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa.
Mhe. Kaminyoge ametoa wito kwa watalamu wa lishe kutoa elimu kwa watendaji wa Kata na Walimu wakuu kuhusu lishe ii kupunguza udumavu pamoja na akina mama wajawazito kujifungua watoto wenye matatizo mbalimbali yakiwemo mgongo wazi na usonji.
Nae Afisa Elimu viafaa na takwimu sekondari Ndg. Mathayo Maigu amesema uvutaji wa sigara na ugoro ni tatizo kubwa kwa kina mama wajawazito hivyo amewaomba watendaji kutoa elimu ili kunusuru akina mama wajawazito kuepuka kujifungua watoto wenye matatizo.
“Lishe isije tu kwa sababu ya kuzuia njaa, iwe lishe inayoweza kuboresha afya ya watoto wetu hasa katika masuala ya akili mtoto anapodumaa hata akili yake haiwezi kuchanganua mambo ndio maana serikali inasisitiza watu wafuate kanuni za lishe ili watu wasiwe na udumavu” amesema Ndg. Mtipa.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ameongeza kuwa unga huo ukisagwa katika mashine zenye virutubisho utaongeza thamani katika lishe ambapo watoto wataweza kufanya vizuri katika masomo yao na kufikili vizuri.
Afisa lishe wa wilaya Bw. Gyunda amewataka watendaji wa kata kuhamasisha wamiliki wa mashine za kusaga mahindi kuunda kikundi ambacho kitawawezesha kupata mashine ya virutubisho ambayo itasaidia watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito kupata unga wenye virutubisho vya madini chuma.
Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Maswa Ndg Athuman Kalage amesema suala la lishe linatakiwa liwe ajenda ya kudumu katika vikao vyote vinavyofanyika ngazi ya Kata ili kufuatilia kwa karibu taarifa za wahudumu wa afya ngazi ya jamii na kutoa elimu zaidi ya lishe.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.