Viongozi wa shirika la maendeleo UNDP kutoka ofisi yao Makao makuu Dar es Salaam wamezulu Wiliyani Maswa kwa ajili ya kutembelea viwanda.
Ziara ya wataalamu hao imefanyika leo tarehe 29.05.2019 kwa kukagua Viwanda vilivyopo Wilayani hapa.
Viwanda vilivyotembelewa ni pamoja na Kiwanda Cha kusindika Viazi lishe kilichopo katika Kijiji Cha Njiapanda Kata ya Isanga, Kiwanda Cha chaki kilichopo mtaa wa Ndilizu mjini Maswa, Kiwanda Cha kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi kilichoko katika kijiji cha Senani, na Ujenzi wa Viwanda vya Chaki na vifungashio katika eneo la Ng'hami.
Wataalam hao kutoka UNDP wamefurahishwa, kuridhishwa na utekelezaji, usimamizi unaofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa katika kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda na katika kutekeleza kauli mbiu ya Mkoa wa Simiyu ya "Wilaya moja bidhaa moja(ODOP)" na kauli mbiu ya Kijiji kimoja bidhaa moja(OVOP).
Maswa ya Viwanda inawezekana wakati huu kwa pamoja tushikamane, tushirikishane tutafanikiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.