Kambi maalumu la kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma katika shule za sekondari mkoani Simiyu lililoanza hapo tarehe 3/4/2018 limelimefungwa rasmi leo terehe 13/4/2018. Kambi hili limefungwa na MKuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akiambatana na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoani Simiyu.
Akifunga kambi hiyo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huu uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu.
Ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali wa elimu walioweza kufanikisha ufanisi wa kambihilo kwa michango yao mbalimbali, amewaomba waendelee kuwa moyo huo kwani unaleta chachu ya maendeleo katika jamii zetu, mkoa wetu na nchi kwa ujumla.
Ametoa zawadi ya vyeti vya kutambua mchango wa wadau waliofanikisha kufanyika kambi hilo. Walimu mahiri nao amewapa zawadi ya vyeti kutambua juhudi na mchango wao wa kuwaweka sawa Wanafunzi hao.
Kupitia ofisi yake ametoa ahadi mbalimbali kutokana na ufaulu utakaopatikana kwenye mtihani unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao; Mwanafunzi atakayeingia 10 bora kitaifa atapata shilingi milioni mbili, Shule itayoingia 10 bora kitaifa itapata shilingi milioni tano, Mwalimu ambaye mwanafunzi wake atapa alama A kwenye somo lake atapata shilingi laki mbili. Aidha wadau mbalimbali pia wametoa ahadi kwa watakaofau vizuri; Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amehaidi kwa Mwanafunzi atakayeongoza kwa kupata daraja I la pointi 3 atampa shilingi laki tano, Bw. Gungu mfanya bihashara mashuhuri Wilayani Bariadi ameahidi Mwanafunzi atakayeongoza mkoani Simiyu atampa Laptop na tiketi ya kwenda na kurudi chuo takapokuwa amechaguliwa na shule itakayoongoza itapewa shilingi milioni mbili.
Kutokana na mafanikio ya kambi hili ametangaza kutakuwepo na kambi la kidato cha nne na darasa la saba miezi ijayo mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.