International Institute of Tropical Agriculture (IITA) kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo kitengo cha Afya ya mimea ( National Biological Control) wametembelea Wilaya ya Maswa na kutoa elimu kwa maafisa Ugani Wilayani hapa juu ya SUMUKUVU na njia ya kupambana nayo.
Sumukuvu nia aina ya sumu inayozalishwa na fangasi au kuvu ambao hukaa kwenye udongo na masalia yaliyooza shambani. Mazao ambayo hushambuliwa zaidi na kuvu hawa ni mahindi na karanga. Sumu hiyo haionekani kwa macho, haina kionjo wala harufu. Vipimo vya maabara pekee ndivyo vinauwezo wa kubaini Sumukuvu. Sumu hii huathiri Wanadamu, mifugo na biashara.
Sumu hii inaweza kuzuiliwakwa njia ya kutumia kanuni bora za kilimo na baada ya kuvuna mazao. Pia tunaweza kutumia mbinu salama na ya gharama nafuu ya kibaiolojia kwa kutumia AFLASAFE itakapoanza kupatikana. AFLASAFE imetengenezwa na kuvu wasiozalisha sumukuvu
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.