Minada ya Senani na Shanwa ni miongoni mwa minada mikubwa iliyopo katika Wilaya ya Maswa ambayo inatoa huduma kwa wafanyabiashara na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya ndani ya Wilaya na Wilaya jirani za Mkoa wa Simiyu na Kishapu ya Mkoa wa Shinyanga lengo ni kufanya biashara ya mifugo, nafaka na bidhaa nyingine nyingi.
Kwa kutambua umuhimu wa minada hiyo katika kuchangia mapato ya Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Maisha Mtipa pamoja na wakuu wa Divisheni na vitengo wametembelea minada hiyo ili kufuatilia ukusanyaji wa mapato katika minada hiyo.
Pia wakiwa katika minada hiyo wamekagua risiti na kuhakikisha wafanyabiashara wote waliopo katika minada hiyo wanalipa ushuru kwa manufaa ya kuongeza mapato ya Halmashauri na taifa kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.