Mkuu wa Divisheni ya elimu ya awali na msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt Lucy Kulon’gwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha shs milioni 348, 500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya mkondo 1 katika shule ya msingi Mwakabeya.
Dkt Lucy ameongeza kuwa mradi huo utasaidia wanafunzi wa kijiji hicho kupata elimu vizuri kwa kuwa kabla ya mradi huo wanafunzi hao wanasomea madarasa mawili tu kuanzia darasa la kwanza mpaka la sita hivyo kusababisha mlundikano wa wanafunzi katika darasa moja.
Aidha amesema kuwa kabla ya kuazishwa kwa shule hiyo kama shule shikizi wanafunzi wa kijiji hicho walikuwa wanatembea umbali mrefu katika vijiji jirani vya Senani, Bushashi na Ipililo kupata elimu huko hivyo ujenzi wa shule hiyo utasaidia wanafunzi wengi kusoma katika shule hiyo.
Amezungumza hayo wakati wa ziara ya kamati ya elimu, afya na maji ilipotembela miradi hiyo na kuona hatua ilipofikia na kuridhishwa na namna ambavyo miradi huyo inatekelezwa kwa weredi.
Nao wajumbe wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti wamempongeza Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu, viongozi na mafundi wote wanaosimamia miradi hiyo kwa kuwa miradi ipo katika hatua nzuri.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Ngulinguli, mradi unaotekelezwa na serikali kupitia mradi wa BOOST shilingi milioni 56,300,000/= zimetolewa na mradi upo katika hatua ya ukamirishaji.
Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ofisi 1 na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Mwawayi ambapo kiasi cha shilingi milioni 76,704,545.54/= zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF).
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.