Kijiji Cha Mwashegeshi kilichopo kata ya Nguliguli ni miongoni mwa vijiji vilivyokuwa na ukosemu wa huduma ya maji safi na salama hivyo kupelekea wananchi wake kutumia maji yasiyo salama na Safi kutokana na changamoto hiyo serikali iliiona adha hiyo na kutoa kiasi Cha shilingi milioni 519 kwa ajili ya kupeleka mradi wa maji katika Kijiji hicho.
Lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama pamoja na kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayotokana na utumiaji wa maji yasiyo salama na pia kutunza chanzo Cha maji ambacho kinasamabaza maji katika mji wa Maswa na vijijini 11.
Kamati ya siasa Wilaya ya Maswa ilifika katika mradi huo kukagua na kuona namna utekelezaji unavyoendelea ambapo wajumbe wa kamati hiyo walitoa pongezi kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi milioni 519 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji katika Kijiji Cha Mwashegeshi
“Nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mhe Rais Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa nia yake na dhamira ya dhati ya kumtua mama ndoo kichwani kwa mradi huu wa maji katika kijiji hiki cha mwashegeshi wenye thamani ya milioni 519 tunapata mradi huu katika kijiji hiki ambao unakwenda kutatua kabisatatizo la upatikanaji wa maji”. Mwenyekiti wa CCM Wilaya
Akizungumza katika ziara hiyo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika eneo la mradi wa tenki la maji ambalo litasambaza maji katika Kijiji hicho Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe Onesmo Makota alisema mradi huo ni mkubwa hivyo amewataka wananchi kuutunza ili udumu kwa muda mrefu
Nae Diwani wa Kata ya Nguliguli Mhe Peter Mathias alimpongeza Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa Fedha kiasi Cha shilingi milioni 519 kwa ajili ya kutatua kero hiyo ambayo ilikuwepo miaka 30 sambamba na hilo pia alitoa pongezi kwa Wabunge wote na Mhe Mkuu wa Wilaya kwa usimamizi na ufatiliaji wa mradi huo mpaka ukaanza.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge alitoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita kwa kutoa Fedha nyingi katika wilaya ya Maswa hususani katika miradi ya maji ambayo inatekelezwa ili ifikapo mwaka 2025 wananchi wawe wamepata maji kwa asilimia 95 mjini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Maswa (MAUWASA) Mhandisi Nandi Mathias alibainisha shughuli mbalimbali ambazo zinatekelezwa katika mradi huo ikiwepo ujenzi wa tenki kubwa lenye ujazo wa Lita laki moja na ulazaji wa bomba kilometa 11.
Aidha aliongeza kuwa katika kuhakikisha bwawa hilo linahifadhiwa Mamlaka hiyo inajenga mbauti kwa ajili ya kunyweshea ng'ombe pamoja na ujenzi wa vituo 6 vya kuchotea maji ambapo mpaka sasa kazi hiyo inaendelea ambapo ikikamilika itanufaisha wananchi wengi.
Mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya Ndg Mwashi Shidile alimshuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwatua akina mama ndoo kichwani kwa sababu wana majukumu mengi majumbani mwao hivyo ujio wa mradi huo utawasaidia sana.
Wakiwa katika ziara hiyo kamati ya siasa Wilaya ya Maswa ilikagua miradi 12 ya Elimu, Afya, maji, barabara pamoja na umeme ambapo kamati hiyo imeridhishwa na miradi yote hiyo na kuomba miradi ambayo haijakamilika ikamilike kwa wakati kutokana na mkataba ulivyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.