Serikali kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu imetoa salaam mbalimbali kwa wananchi siku ya Baraza Maalumu la kupitia Hoja za mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali za mwaka 2018/2019. Salam hizo zimewasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Ndugu Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.
Ameshukuru ushirikiano uliopo kati ya waheshimiwa Madiwani na Wataalamu katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali wilayani hapa. Kwa ushirikiano huo pia umesifia uthubutu wa Baraza hilo kuanzisha kiwanda cha Chaki, Ungalishe, Viatu na cha kukoboa na kupanga madaraja ya mchele.
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imepata Hati safi kutokana na Ukaguzi uliofanyika. Pamoja na kupata Hati safi kuna Hoja 26 zilizoibuliwa ambazo leo zimepitiwa na kuthibitishwa majibu yote.
Kwa msisitizo ameshauri Madiwani wakiambatana na Wakuu wa Idara watembelee miradi yote ya maendeleo ya kimkakati kabla ya Baraza kuvunjwa ili waifahamu kwa upana wake.
Kutokana na janga lililopo Duniani sasa, amesisitiza kuendelea kufikishwa elimu kwa Wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa wa corona ikiwa ni pamoja na kutofanyika sherehe za kimila zinazofanywa mara kwa mara katika maeneo yetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.