• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

RC Nawanda aipongeza Maswa kwa usimamizi mzuri wa miundombinu ya Elimu

Posted on: October 28th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda ametoa kongole kwa viongozi wa Wilaya ya Maswa kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miradi ya elimu inayoketelezwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Maswa.

Mkuu wa Mkoa alisema hayo kwa nyakati tofauti wakati akikagua miradi ya ujenzi wa shule mpya 2 za  Sekondari zilizopo Kata ya dakama na kulimi ambapo ujenzi huo umegharamiwa na serikali kupitia mradi wa kuimarisha Elimu ya sekondari (SEQUIP ) ambapo kila shule ilipata kiasi cha shilingi milioni  584,200,000/=  na ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji.

Aidha Mhe Dkt Nawanda alitembelea ujenzi wa shule mpya ya msingi Jija A yenye mikondo miwili na kuwapongeza Wilaya ya Maswa kwa kuweka fensi katika shule ya awali ili kuwalinda watoto wa chekechea ambao watasoma hapo ambapo, pia alikagua ukarabati wa shule ya msingi Malampaka.

Aidha alitembelea ujenzi wa jengo jipya la Utawala ambalo linajengwa katika Kitongoji cha Ng'hami Kata ya Nyalikungu ambapo mradi huo upo katika hatua ya msingi ambapo serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi huo awamu ya kwanza (Phase one) sambamba na ujenzi wa nyumba ya mtumishi ya 2 in 1 katika shule ya sekondari Mashimba serikali kuu  ilitoa kiasi cha shilingi milioni 100 ambapo ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji.

Mkuu wa Mkoa alimshukuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha nyingi ambazo zimewezesha wananchi wa maeneo hayo kupata miundombinu ya Elimu ambayo itawasaidia watoto hao kusoma katika Mazingira mazuri.

Dkt Nawanda amewashukuru wananchi wa Maswa kwa utoaji wa chakula mashuleni ambapo katika Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Maswa inaongoza kwa utoaji wa chakula shuleni  kutokana na sifa hizo amewataka waendelee kuchangia chakula ili watoto wao wasome vizuri na kufaulu mitihani yao kwa wastani unaotakiwa.

Katika hatua nyingine Mhe. Dkt Nawanda amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema pindi mvua za El-nino zitakapoanza kwa kuhama maeneo ambayo yatakuwa hatarishi na amesisitiza wananchi kutokuuza chakula chote katika kipindi hicho

Ametoa wito kwa viongozi wote kuanzia ngazi ya Wilaya mpaka Kata kuandaa mpango wa kutenga  maeneo ya kuwahifadhi wananchi pindi mvua zitakapozidi na kusababisha maeneo yao kuwa na maji mengi.

Akiwa Wilayani Maswa Mkuu wa Mkoa amezungumza na wanachi katika maeneo tofauti alipokuwa akikagua miradi hiyo na kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wananchi wa maeneo hayo sambamba na hilo amewataka wananchi kuchangamkia fursa kwa kuchukua mbegu za pamba ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa bure kwa ajili ya wakulima wote kulima kwa wingi zao hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amempongeza Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha nyingi kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ya maji, umeme, barabara, Elimu na afya  ambapo wananchi wa Maswa wanapata huduma hizo vizuri.



Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.