Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Dkt Yahaya Nawanda amewapongeza wanawake kwa kazi wanayoifanya katika nyanja mbalimbali kwa kushirikiana na kupendana ili kukuza maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu.
Mhe Dkt Nawanda amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo katika Mkoa wa Simiyu yaliadhimishwa wilayani Meatu na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya zote.
Mkuu wa mkoa amesema maadhimisho hayo hufanyika kwa lengo la kutathmini sera, mipango kwa kuweka usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri katika tasnia mbalimbali kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Dkt Nawanda amesema serikali inatambua mchango wa kina mama ambapo serikali ya Mkoa wa Simiyu imetenga shilingi milioni 579 fedha kutoka mapato ya ndani kwa mwaka 2021/2022 ambazo zimetolewa kwa vikundi vya kinamama 133. Pia Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan ametoa fedha kiasi Cha shilingi 579 katika Mkoa wa Simiyu kusaidia akina mama.
Aidha, amesisitiza kuwa katika Mkoa wa Simiyu vikundi vya wanawake 102 kutoka Wilaya zote vilipewa mkopo katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 shilingi 579,975,458 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
"Ukimpa fedha mwana mama una uhakika wa kurudisha kwa asilimia mia moja na Nichukue nafasi hii kuwaambieni wanaorudisha mikopo vizuri katika mkoa wetu ni ile mikopo inayoenda kwa kina mama hongereni akina mama" amesema Dkt Nawanda
Pia Dkt Nawanda ameongeza kuwa vikundi vya wanawake 1485 vimepata mafunzo mbalimbali yakiwepo ya ujasiliamali na elimu nyingine na Mkoa utaongeza nguvu ili kufikia mwakani kuwe na vikundi zaidi ya 2000 mpaka 3000 vitakavyopata mafunzo.
Pia Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kutoa elimu kwa kupinga ukiukwaji wa jinsia kwa kupinga Mila zote zinazokiukwa katika jamii.
Baadhi ya akina mama wa Wilaya ya Maswa wakifuraia siku ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani tarehe 08/03/2023 yaliyoadhimishwa kimkoa Wilayani Meatu
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.