Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za serikali
Dkt Nawanda amesema hayo katika kikao Cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa leo tarehe 20.06.2023 kilichokuwa na ajenda ya kujadili hoja ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG).
Mkuu wa Mkoa amesema hoja zote zilikuwa 98 ambapo hoja 66 zimepata majibu na 32 zinaendelea kutekelezwa ili zifungwe.
"Nichukue nafasi hii kumpongeza CAG kwa kazi nzuri anayoifanya kwa hakika amefanya kazi nzuri sana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaendelea kushirikiana na wewe" amesema Dkt Nawanda.
Pia Mkuu wa Mkoa amewasisitiza wakuu wa Idara kusimamia vizuri majukumu yao ili kuepuka kuzalisha hoja mpya, sambamba na hilo pia amemwagiza mkuu wa Kitengo cha Fedha kuwasisitiza wakusanya Mapato kupeleka Fedha benki mara baada ya kukusanya fedha hizo ili kuepuka watumishi hao kupoteza mapato ya Halmashauri na wao kuingia katika matatizo ambayo yatawasababishia shida katika utumishi wao.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg Prisca Kayombo amewashukuru viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa ushirikiano waliouonesha kwa kuwezesha ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kutekeleza hoja zote kwa asilimia 100%.
Pia Ndg Kayombo amewaomba waheshimiwa madiwani na wataalamu kuendelea kufanya kazi zaidi ili kuitoa Maswa mahali ilipo na kuifikisha sehemu nzuri ili kuweka rekodi nzuri.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi wilaya ya Maswa Mhe. Onesmo Makota amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Katika wilaya ya Maswa.
" Kwa niaba ya Chama Cha Cha Mapinduzi wilaya nikupongeze wewe kwa namna ambayo unachapa kazi hotuba yako Mkuu wa Mkoa imegusa maeneo yote kwenye kuelekeza , kuonya, kushauri hongera sana". Amesema Makota
Aidha Mhe. Makota amewapongeza watendaji wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa pamoja na waheshimiwa Madiwani kwà kupata hati safi ambayo imezalishwa na utendaji mzuri wa watumishi hao katika kutimiza majukumu yao kwa kila mtu katika eneo lake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Maswa Mhe. Paul maige amesema umoja na mshikamano ndio utaimalisha mapato katika Halmashauri ya Maswa na kuondoa hoja ambazo zinapatikana katika Halmashauri na kutimiza matakwa ya kisheria.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.