Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo leo 09 Januari, 2025 ametembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kupitia BOOST na SEQUIP katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Akiwa katika ziara hiyo Katibu Tawala Mkoa amekagua miradi 3 ya BOOST ambayo ni shule mpya ya msingi majengo iliyopo katika Kata ya Shishiyu, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Jija B iliyopo Kata ya Jija, ambapo ujenzi huo upo katika hatua ya ukamilishaji.
Pia amekagua shule mpya ya msingi Butalwa iliyopo kata ya Jija, pamoja na mradi mmoja wa SEQUIP ambao ni shule ya sekondari Kulimi Mkuyuni iliyopo Kata ya Kulimi.
Aidha ametoa pongezi kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi hiyo pamoja na chama cha Mapinduzi kwa ushirikiano mzuri ambao umewezesha miradi hiyo kukamilika.
Pia Bi. Kayombo ametoa pongezi kwa viongozi wote wa wilaya kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo kwa kuwa imekamilika kwa ubora.
Sambamba na hilo amewataka walimu wakuu wote wanaosimamia shule hizo kuhakikisha wanapanda miti kuzunguka maeneo ya shule na kusimamia wanafunzi kuitunza miundombinu hiyo ili idumu na kutumika kwa muda mrefu.
Kukamilika kwa shule hizo kumesaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, kupunguza msongamano wa wanafunzi pamoja na wanafunzi kutotembea ubari mrefu kutatufa elimu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.