Benki ya NMB tawi la Maswa imekabidi vifaa vya ujenzi katika Shule ya Sekandari Mataba na Shule ya Msingi Iyogelo ikiwa ni kutoa mchango wa kuunga nguvu za wananchi ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hizo.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mabati, Mifuko ya Saruji, Mbao na Misumari.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa na meneja msaidizi wa NMB kanda ya Magharibi ndugu James Katambo akiongozwa na meneja wa tawi Benki ya NMB Maswa. Wamemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambaye pia amekabidhi uongozi wa shule zote mbili kulingana na mahitaji.
Kwa pamoja karibuni tuijenge Maswa yetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.