Mwenge wa uhuru umetembelea, umekagua na kupanda mti katika mradi wa kitalu cha miti, hifadhi ya Mazingira na vyanzo vya maji katika Kijiji cha Zanzui Kata ya Zanzui ambapo mradi huo una thamani ya Shilingi 227,200,000/=.
Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kushirikiana na Mamlaka ya bonde la ziwa Victoria kwa msimu wa 2019/2020 walipanda miti 10000 katika eneo la kuzunguka bwawa la New sola.
Akisoma taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Afisa Nyuki Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Salum Kuzenza amesema Wilaya ya Maswa imepanda miti 241,014 katika maeneo mbalimbali zikiwemo taasisi za umma, watu binafsi pamoja na eneo la vyanzo vya maji ambapo lengo likiwa ifikapo mwisho wa mwaka 2023 miti 1,500,000 iwe imepandwa katika Wilaya ya Maswa.
Pia Ndg. Kuzenza ameongeza kuwa mradi huo utasaidia katika utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji kwa kuhifadhi maliasili, kupunguza kiwango cha gesi ukaa na kuongeza makazi ya viumbe hai sambamba na hilo pia kuanzishwa kwa kitalu hicho cha miti kitasaidia kusambaza miti maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Maswa ili kupunguza changamoto ya kimazingira inayotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Nae mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Ndaki amewataka wananchi wa eneo hilo la mradi kutunza vyanzo vya maji kwa kuwa wanapata faida katika chanzo hicho kuweka mizinga ya nyuki ili iwasaidie.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg. Abdalla Shaib Kaim akipata maelezo kuhusu kitalu cha miti
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg. Abdalla Shaib Kaim akikagua hifadhi ya Mazingira pembezoni mwa Bwawa la Maji Zanzui
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg. Abdalla Shaib Kaim akipanda mti katika eneo la kitalu cha miti Zanzui
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg. Abdalla Shaib Kaim akionyeshwa aina mbalimbali ya miche iliyopandwa katika kitalu cha miti
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.