Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amewaongoza watumishi wa Wilaya ya Maswa katika zoezi la upandaji wa miti na Usafi wa Mazingira lililofanyika tarehe 24 April 2024 katika hospitali ya Wilaya ya Maswa ikiwa ni kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.
Mhe Kaminyoge amesema mwaka huu nchi ya Tanzania inaadhimisha matukio matatu ambayo ni maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, maadhimisho ya kuanzishwa rasmi kwa jeshi la wananchi wa Tanzania 1964 na miaka 60 ya mwenge wa uhuru tangu uanze rasmi kukimbizwa.
Kupitia maadhimisho hayo mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa kila mtumishi na Taasisi kuhakikisha wanapanda miti ili iwe kumbukumbu kwao na taasisi kuhusu Muungano pamoja na hilo amewataka wakandarasi wanaotengeneza barabara kupanda miti kandokando ya barabara.
Pia Mhe. Kaminyoge amewashukuru watumishi kwa kuendelea kutekeleza majukumu ya serikali kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kuwa mchango wao ni muhimu katika jamii hivyo amewaomba kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa moyo wao wote, nguvu, na akili ili wananchi waweze kutambua uhalali wa serikali yao.
Katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzaniaya Wilaya ya Maswa imepanda Zaidi ya miti 1217 katika shule ya Sekondari Nyongo, Hospitali ya Wilaya ya Maswa na maeneo mbalimbali zikiwepo taasisi na watu binafsi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania "Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu"
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.