Jana tarehe 30/1/2017 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe: Anthony J. Mtaka alitembelea na kukagua mashamba mawili ya Pamba katika kijiji cha Buyubi Wilayani Maswa. Katika ziara hiyo alipokea changamoto za upungufu wa Dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia zao hilo. Katika musimu wa kilimo cha mwaka huu Wilaya ya ilikuwa na lengo la kulima Hekta 50,629 lakini kutokana na uhamasishaji uliofanyika na muitikio wa wananchi hadi sasa Hekta 70,070 za zao la Pamba zimeishalimwa. Kutokana na idadi hiyo ya hekta dawa ya kuulia Wadudu waharibifu wa zao hili inayohitajika ni Acrepack 377400 lakini zilizopokelewa hadi sasa ni acrepack 122900 na pungufu ni acrepack 254500.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.