Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dr. Frederick D. Sagamiko ameungana na wananchi wa kijiji cha Mwabagalu kukomboa shamba la kijiji lenye ukubwa wa ekari 25 lililokuwa limeuzwa kinyemela na mwanakijiji akishikiliana na baadhi viongozi wa kijiji hicho.
Akiongozwa na Wananchi wa kijiji hicho amekagua shamba hilo. Shamba hilo la kijiji liliuzwa kinyemela bila wananchi kijijini hapa kushirikishwa wamesema wananchi wakati wakiongea na Mkurugenzi Mtendaji katika eneo la shamba hilo. Baada ya ukaguzi huo Mkurugenzi Mtendaji amekubaliana na Wananchi kuwa shamba hilo ni mali ya kijiji na si mali ya mtu binafsi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.