Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amesema Mwenge wa Uhuru utatembelea, utakagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.5 katika Wilaya ya Maswa.
Amesema hayo wakati akipokea Mwenge huo kutoka Wilaya ya Meatu katika Kijiji Cha Sangamwalugesha kilichopo Kata ya Sangamwalugesha leo tarehe 26 Julai, 2023 ambapo Mkuu wa Wilaya amesema Mwenge huo utakimbizwa Km. 135 katika Tarafa 3 Kata 36 na Vijiji 120 vya Maswa.
Kwa upande wake mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim amesema lengo la Mwenge wa uhuru ni kuhamasisha na kuelimisha wananchi katika shughuli mbalimbali zinazofanyika ikiwepo Elimu juu ya Athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Pia Ndg. Kaim ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwepo Afya, Elimu, Maji Safi na salama pamoja na miundombinu ya barabara.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge (kulia) akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu 26/7/2023 katika Kijiji cha Sangamwalugesha
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.