Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa limeridhia azimio la kufuta Mamlaka ya mji mdogo wa Maswa na kuridhia azimio la kuanzisha kwa Halmashauri mbili za Maswa Mashariki na Maswa Magharibi ili kusogeza huduma kwa wananchi za kiuchumi, kisiasa na kijamii
Hayo yalisemwa na Waheshimiwa Madiwani katika kikao Cha baraza la Madiwani Cha robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Mamlaka ya mji mdogo Maswa ilianzishwa mwaka 2010 kufatia tangazo la serikali la GN NO: 287 la mwaka 1993 lengo likiwa ni kusimamia maendeleo ya shughuli za kiuchumi.kisiasa na kijamii,
Jukumu likiwa ni kusimamia mpango wa bajeti matumizi ya kawaida, kudumisha mahusiano mazuri kati ya Mamlaka ya mji mdogo na Halmashauri ya Wilaya pamoja na kusimamia Usafi wa mji katika kaya, mitaa, vitongoji na sehemu za umma.
Tangu mwaka 2010 Hadi Sasa ni takribani miaka 13 Mamlaka ya mji mdogo wa Maswa umeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ili Mamlaka ya mji mdogo iweze kuwa Halmashauri ya mji ni lazima iwe na eneo la Kata 12 lakini mpaka sasa Ina Kata 4 tu hivyo kutokizi vigezo hivyo.
Pia Mamlaka hiyo imeshindwa kusimamia vyanzo vya mapato na kuendelea kuipa mzigo Halmashauri ya Wilaya kwa kuendelea kulipa posho kwa watumishi wa Mamlaka ya mji mdogo sambamba na hilo pia kutokusimamia vizuri Usafi wa mji na kusababisha magonjwa ya mlipo.
Kutokana na mambo yote hayo Mamlaka ya mji mdogo tangu kuanzishwa kwake imeshindwa kufikia malengo ya kuanzishwa kwake kwa kutekeleza kwa ufanisi majukumu iliyokabidhiwa kwa Mamlaka hiyo hivyo baraza rikaridhia kufutwa Rasmi kwa mji huo na kuanzishwa Halmashauri mbili.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw. Maisha Mtipa alisema Madiwani kwa kauli moja wameridhia azimio la kuvunja Mamlaka ya mji mdogo kwa kuwa Mamlaka hiyo imekosa sifa kwa sababu imeanzishwa muda mrefu lakini Bado haijaweza kujitegemea.
Aidha Bw. Mtipa alisema Mamlaka hiyo imeendelea kuongeza mzigo kwa Halmashauri ya Wilaya kwa kuwa Halmashauri Ina Kata 36, vijiji 120, vitongoji 510 ambapo Mamlaka ya mji ilikuwa na vitongoji 40 lakini hawakuweza kufanikisha kuanzishwa kwa Halmashauri ya mji.
"Wajumbe wakaona afadhali ivunjwe kwa sababu inakosa sifa ya kuwa Halmashauri, pia wajumbe nao wamepitisha kwa kauli moja kuanzishwa kwa Halmashauri mbili kutokana na vigezo vya majimbo ambapo Jimbo la Maswa Mashariki lina Kata19 na Jimbo la Maswa Magharibi lina Kata 17 ili kusogeza huduma kwa jamii." Alisema Mkurugenzi Mtendaji
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa Ndg Onesmo Makota amesema kuvunjwa kwa Mamlaka ya mji mdogo na kuanzisha kwa Halmashauri mbili kutasaidia kusogeza karibu huduma kwa wananchi
"Ni sahihi kabisa kuigawa Halmashauri ya Maswa kwa kuwa ni kubwa na Ina majimbo mawili Kata 36, lakini nchi hii Kuna Wilaya Zina Kata 4 au 3 kwa hiyo Kata 36 kuzigakuwa Halmashauri mbili Bado ni sawa, tunasogeza huduma kwa wananchi ili wananchi waweze kufika maeneo ya kupata huduma kwa urahisi."Alisema Mhe. Makota
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe Paul maige alisema lengo la kuwa na mji mdogo ni kusogeza huduma kwa wananchi lakini mapungufu yaliyojitokeza ya dhamira ya kuwa na Mamlaka ya mji
"Mapungufu yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na upungufu wa mapato kwenye eneo la Mamlaka lakini pia na suala la miundombinu kwa sababu hatua hiyo inachelewa kufikia Halmashauri ya mji na Halmashauri ya Wilaya imekuwa na mzigo wa kuendesha Mamlaka ya mji mdogo."alisema Mwenyekiti wa Halmashauri
Ameongeza kuwa ili kuweka tija kwa kuwa na wigo mpana wa kupeleka Fedha za maendeleo baraza la mji mdogo linapaswa kuvunjwa ili kupata Fedha za kupeleka kwa wananchi kwa ajili ya maendeleo sambamba na hilo kuanzishwa kwa Halmashauri mbili kutusaidia kuwa karibu na wananchi ambapo mchakato ukikamilika utasaidia ongezeko la ajira.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.