Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amesema tatizo la maji katika mji wa Malampaka litakuwa historia kwa sababu serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa Fedha kwa ajili ya kuleta maji mji wa Malampaka.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa maelekezo ya Waziri Mkuu kuhusu mkataba wa kutoa maji Hungumalwa kuja Malampaka tayari yametekelezwa ambapo mkataba umesainiwa na Waziri wa Maji ili maji hayo yaanze kuletwa Malampaka kwa kuwa tatizo la maji ni kubwa
"Wakandarasi wanaanza kuleta maji ya ziwa Victoria kutoka kwenya Bomba la KASHIWASA linalopeleka maji Shinyanga, Tabora na Nzega kwa hiyo maji yetu Wanamalampaka Sasa baada ya miezi minne au mitano maji yatakuwa yameingia na kutakuwa na tenki kubwa pamoja na Bomba la kuleta maji hapa ambalo litasambaza maji maeneo mengine ikiwepo Mataba na Nyabubinza". Amesema Kaminyoge.
Pia Mhe Kaminyoge amesema atakuwa bega kwa bega na wananchi kufuatilia kwa karibu mradi huo wa maji ili uweze kukamilika kwa wakati na watu wa Malampaka waweze kutumia maji hayo na kuondokana na kero hiyo.
Aidha mkuu wa wilaya ametoa wito kwa watu wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Maswa (MAUWASA) kuhakikisha wanakamilisha haraka ujenzi wa tenki ambalo linajengwa Malampaka ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji kwa miezi hiyo ambapo maji ya ziwa Victoria bado hayajafika katika mji wa Malampaka.
Mkuu wa Wilaya amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa ulizi na usalama katika mji wa Malampaka wakati akilishukuru jeshi la sungusungu kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendeleza amani na utulivu katika wilaya ya Maswa kwa sababu matukio ya uhalifu yamepungua kwa kiasi kikubwa katika wilaya ya Maswa ili kuwasikiliza wananchi kero zao na kuwaeleza mafanikio ambayo serikali imeyafanya.
Pia Mhe Kaminyoge ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa inazozifanya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma mbalimbali za kijamii ikiwepo Elimu, Barabara na Afya.
Pia amewataka wananchi kuiamini serikali kwa kazi kubwa inayoifanya ya kuleta maendeleo ikiwepo Barabara ambayo itajengwa kwa kiwango cha Rami kutoka Maswa Lalago Sibiti mpaka Arusha ili kuhakikisha wananchi wanakuza uchumi wao.
Kwa upande wao wananchi wamempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuongea nao na kusikiliza kero zao ambapo wameahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali kwa kazi kubwa ya kuwaletea mandeleo wananchi wa Maswa.
Ujenzi wa Tanki la Maji Malampaka
Wananchi wa Malampaka wakiwa kwenye Mkutano na Mkuu wa Wilaya
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.