• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Mafunzo ya UWaWa yawe chachu ya maendeleo katika elimu

Posted on: March 18th, 2023

Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt Lucy Kulong'wa alisema mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kutatua changamoto kwa kuhamasisha jamii kuunganisha na kuwa na ushirikiano ili kuleta  maendeleo ya jamii nzima katika  Kijiji, Kata na Wilaya.

Aliyasema hayo wakati akifunga  mafunzo  ambayo yalifanyika kwa siku tisa katika makundi tofautitofauti katika shule ya msingi Shanwa.

Mafunzo hayo  yaliaandaliwa na mradi wa shule Bora yenye lengo la kuanzisha uhusiano baina ya wazazi na walimu  ili kurahisisha shughuli za ujifunzaji hivyo kutoa matokeo chanya kitaaluma na elimu Bora kwa watoto  .ambapo wanamafunzo 300 wamepata Elimu ya ushirikiano baina ya wazazi na walimu yaani  (UWaWa)

Pia Dkt Kulong'wa alisema kuna changamoto za kimazingira ya kujifunzia ikiwepo uhaba wa madarasa na vyoo hivyo amewataka Walimu Wakuu, Maafisa Elimu Kata na Wenyeviti wa Kamati za Shule kuhamasisha jamii kwa kuwa wamepata mafunzo na miongozo ambayo itawawezesha kutekeleza majukumu yao.

"Mimi naomba nisisitize mkatengeneze mazingira mazuri kwa ajili ya watoto wetu Kuna mambo ya KKK  na wanafunzi Wanashindwa kujifunza kusoma na kuandika kutokana na ule mlundikano wa  wanafunzi wanakuwa wengi lakini madarasa ni machache naomba haya tuliyoyapata tukayafanyie kazi sisi tutakuja kwa ajili ya ufuatiliaji ili tuone je! Kile mlichojifunza hapa mmekifanyia kazi?"

Aidha aliwataka Wenyeviti kuwapa ushirikiano walimu kwa kuwa Wana jukumu la kulea watoto shuleni hivyo ameiomba jamii kuwathamini Walimu na ameitaka jamii kuepuka migogoro badala yake kuwe na upendo baina ya walimu na wanafunzi ili waweze kufanya kazi yao vizuri.

Kwa upande wake Afisa  Mradi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambaye pia ni Afisa Elimu Taaluma Msingi Ndg Neema Makundi alisema mafunzo hayo yalihusisha ushikikishwaji wa mzazi na mwalimu tendo la mtoto kujifunza linahitaji uwepo ushirikiano wa mzazi na walimu, mahusiano mazuri ili kufanikisha tendo zima la utoaji wa Elimu.

Pia Ndg Makundi alisisitita kuwa mafunzo hayo yalilenga kuanzisha uhusiano baina ya wazazi na walimu ili kutoa Elimu iliyo Bora kwa watoto wetu na kwa manufaa ya watoto, Kata na Wilaya.

Nae mwenyekiti wa kamati ya shule kutoka Badi Ndg Andrea Kapene  aliishukuru serikali kwa kuwaletea mafunzo hayo kwa kuwa amejua kuwa shule ni mali ya jamii hivyo itakuwa chachu ya maendeleo katika jamii na ameomba mafunzo hayo yaendelee kutolewa zaidi kwa kuwa yatasaidia kuleta faida kwa wazazi.


Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.